SERIKALI imesema sekta ya utalii nchini imepiga hatua kubwa baada ya kushinda nafasi ya nne barani Afrika kwa kuingiza mapato mengi ya utalii ikitanguliwa na Afrika Kusini, Misri na Morocco.
Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk Hassan Abbas leo jijini Dodoma katika mkutano wake na wandishi wa habari uliolenga kutoa ufafanuzi katika mambo mbalimbali nchini ikiwemo Utalii, Uchumi na Elimu.
Dk Abbas amesema ripoti ya Taasisi maarufu za Utalii ya mwishoni wa mwaka jana, imeonesha kuwa kwa mwaka 2018 Tanzania iliingiza Dola za Marekani Bilioni 2.43 kutoka Dola Bilioni 2.19 za mwaka 2017.
Amesema kwa miaka mitatu iliyopita mifumo ya kodi iliimarishwa huku baadhi ya watu wakatishia kuwa watalii watakimbia nchini, lakini wameongezeka zaidi na kuchangia kukua kwa uchumi.
" Shirika la utangazaji la kimataifa (CNN) katika taarifa ya Novemba, 2019, inasema Tanzania imekua ni nchi ya kwanza kuwa na maeneo mazuri na yakuvutia na kutembelea kuliko nchi zote za afrika," Amesema Dk Abbas.
Kwa upande wa makusanyo ya mapato, Dk Abbas amesema moja ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kusimamia mifumo ya kimageuzi ambayo sasa imeanza kuleta mafanikio makubwa na ya kihistoria nchini.
Amesema kwa miaka mitatu sasa habari kubwa katika mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano katika ukusanyaji wa mapato kwa mwezi ilikuwa ni kutoka Sh.Bilioni 850 mwaka 2015 hadi Sh.Trilioni 1.3.
“ Leo ninayo furaha kulitangazia rasmi Taifa kuwa kutokana na juhudi kubwa zilifanywa na Serikali kupitia TRA na Idara nyingine za Serikali, wastani wa mapato ya kodi kwa mwezi kati ya Julai-Disemba, 2019, umepanda na sasa ni sh. Trilioni 1.5 kwa mwezi na kuna mwezi tuliwahi kukusanya hadi Trilioni 1.7," Amesema Dk Abbas.
Akizungumzia sekta ya madini madini hasa mauzo ya nje ya madini taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ya Novemba, 2019, Takwimu zinaonesha kuwa mauzo ya bidhaa zisizo kuwa zile za kawaida yameongezeka kwa asilimia 31.0 kwa sababu kubwa mbili muhimu:
Moja alitaja kuwa ni Kuongezeka kwa mauzo ya dhahabu kwani Serikali imechukua hatua ya kuanzisha masoko ya madini na kuzuia uuzaji holela na utoroshaji wa madini.
No comments:
Post a Comment
Kwa mawasiliano;
Eliud Rwechungura
0759646339
eliudrwechungura98@gmail.com
Karagwetv@gmail.com
Endelea kutufatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii
instagram: karagwetv
Facebook:karagwetv