Askofu Dk. Benson k. Bagonza
HEKIMA, UMOJA NA AMANI HIZI NI NGAO ZETU
''Serikali ikaomba mkopo Benki ya Dunia,
Huyu kaandika barua Benki ya Dunia kulalamika na kushauri mkopo usitolewe,
Mwingine akakemea na kuhukumu kuwa wanaoandika na kusema wanaichafua nchi.
Hili ni somo kamili la URAIA darasa la saba, Civics kidato cha tatu, history paper two kidato cha tano.
Kwamba:
1. Kuna tofauti kati ya nchi na serikali. Ziko nchi zisizo na serikali, ziko nchi zina serikali mbili hata tatu, na serikali huja na kupita. Nchi hubaki.
2. Kuna tofauti kati ya Rais na serikali. Kuna nchi zina rais lakini hazina serikali; kuna nchi zina kitu kinaitwa serikali lakini hazina Rais. Kwa hiyo waweza kumkosoa Rais lakini usiikosoe serikali. Waweza kuikosoa serikali lakini usimkosoe Rais.
3. Mungu wetu ni mkarimu sana. Ameumba watu na kuwapa hata utashi wa kumkataa yeye aliyewaumba. Hata kwa nchi moja, wapo watu mbalimbali:
Kuna watu wanaweza kuipenda nchi wasiipende serikali.
Kuna watu wanaweza kuipenda serikali wasimpende rais.
Kuna watu wanaweza kumpenda rais wasiipende nchi.
Kuna watu wanaweza kukipenda chama tawala wasiipende serikali.
Kuna watu wanaweza kumpenda rais wasikipende chama chake.
Kuna watu wanaweza kukipenda chama wasimpende kiongozi wake.
Kuna watu wanapenda niandikayo lakini wananichukia mimi!
Kuna watu wananipenda mimi lakini wanachukia niandikayo!
Hali kadhalika, kuna wanasiasa wengi wanapenda kura zetu lakini hawapendi mambo yetu.
Ndiyo maana jukumu kuu la kiongozi ni kuwaleta watu pamoja, kuwafanya kuvumiliana. Hakuna kazi ya hatari niijuayo kama ya kuwafanya watu wafikiri kwa njia moja, wafanane wanachopenda na kuchukia na kuwa na mtazamo mmoja kuhusu nchi na serikali yake.
Daima tukumbuke, Kila penye mitume 12, Yuda Iskariote lazima awepo. Na U-Yuda daima umo ndani si nje. Bila Yuda, utume wa kundi lile ungekuwa mgumu.
Mwisho wa siku, bora aliyeandika kuliko wanaofikiri kama yeye na hawaandiki na wamo ndani ya serikali.'' Askofu Dk. Benson k. Bagonza
No comments:
Post a Comment
Kwa mawasiliano;
Eliud Rwechungura
0759646339
eliudrwechungura98@gmail.com
Karagwetv@gmail.com
Endelea kutufatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii
instagram: karagwetv
Facebook:karagwetv