Semina hiyo
imezinduliwa leo Mei 17, 2021 katika ukumbi wa Tripple P, Omurushaka Karagwe
Kagera na itatolewa kwa kata zote 23 za wilaya ya Karagwe kwa kuwafikia
wanawake wajasiriamali 300 ambao ni wawakilishi wa vikundi wanaotegemewa
kupeleka elimu hii kwenye vikundi vyao ili kuwafikia wajasiriamali zaidi ya
4,000 wa Karagwe ili kuleta tija kwenye Biashara zao.
Wakati
akifungua Semina hiyo, Afisa biashara mkoa wa Kagera, kwa niaba ya Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kagera, Bw. Issaya Tendegu amewataka wanawake wajasiriamali
wa wilaya ya Karagwe kulima kilimo chenye tija kwa kutumia mbegu bora ambazo
zinaongeza thamani ya mazao katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Aidha, Bw.
Issaya Tendegu amezitaja fursa nyingi za kibiashara zilizopo wilaya ya Karagwe
na kutoa ufafanuzi wa fursa kubwa ya kijiografia ya Karagwe kuwa moja kati ya
wilaya iliyopo mpakani mwa Tanzania na nchi nyingine za jirani kama Uganda,
Rwanda na Burundi.
Nae
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mama Alaska Jamii, Bi. Jennifer Bashungwa, ameeleza
semina itakavyowasaidia akina mama wajasiliamali kutambua na kufahamu sheria za
kufanya biashara mipakani zitakazowasaidia kunufaika na soko la Jumuiya ya
Afrika Mashariki. Kupitia semina hizi za biashara, wanawake wajasiliamali wa wilaya ya karagwe
watajengewa uwezo na uelewa wa kukuza biashara na kutambua fursa za masoko
yaliyowazunguka.
Taasisi ya
Mama Alaska Jamii imekua ikitoa mafunzo ya biashara kwa makundi mbalimbali ya
wajasiliamali wakiwemo Mama Lishe wa Mkoa wa Dar es salaam na wakulima wa zao
la mpunga wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
No comments:
Post a Comment
Kwa mawasiliano;
Eliud Rwechungura
0759646339
eliudrwechungura98@gmail.com
Karagwetv@gmail.com
Endelea kutufatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii
instagram: karagwetv
Facebook:karagwetv