WAZIRI ZUNGU AMEWAAGIZA WATUMISHI WAFANYE KAZI KWA BIDII


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu amemtaka kila mtumishi katika Ofisi hiyo kuwajibika ipasavyo mahali pa kazi na kuepuka kujihusisha na vitendo visivyokuwa vya kimaadili.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo.


Zungu ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo ambapo aliwakumbusha kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kwa dhati kuimarisha utendaji kazi ili kufanikisha dhana ya Tanzania ya viwanda.

“Ninafahamu kwamba watumishi wana malalamiko yanayohusu kutopandishwa vyeo kwa muda mrefu na upungufu wa watumishi katika Idara na Vitengo, malalamiko haya ni mtambuka katika Wizara zote kwani yametokana na uhakiki wa vyeti vya elimu ya sekondari na ualimu zoezi lililoendeshwa na Serikali kuanzia mwaka 2016. Ninawasihi muwe na subira wakati Serikali ikiimarisha mifumo yake ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu,” alisisitiza.

Aidha, Waziri Zungu alibainisha kuwa Baraza la wafanyakazi ni jukwaa muhimu mahali pa kazi kwani ni kiunganishi kati ya Menejimenti na Wafanyakazi hivyo aliwataka kuendeleza ushirikiano ili kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu ya Ofisi na Taifakwa ujumla.

“Watumishi wenzangu hakikisheni mshahara mnaopewa mnautendea haki! Msitake kupata mshahara wa bure! Fanyeni kazi kwa bidii” Zungu alisisitiza.

Aliongeza kuwa kuwepo kwa Mabaraza ya Wafanyakazi katika Taasisi ni takwa la Kisheria kwa madhumuni ya kuishauri Serikali katika ngazi za Idara na Ofisi ambapo malengo yake ni  kuhakikisha kuwa majukumu yanatekelezwa ipasavyo, kulinda haki na wajibu wa waajiri na wafanyakazi, kutoa ushauri kuhusu kujenga mazingira bora ya kazi, maslahi ya watumishi na kusimamia haki na ustawi katika sehemu za kazi.

Aliwakumbusha kuwa wajibu wa Mabaraza haya kama vyombo vya ushauri na usimamizi ni kuhakikisha kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao na kuzingatia maadili ya utumishi wao ili kuleta matokeo chanya katika utendaji kazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo baada ya kufungua mkutano 
Agenda na madhumuni ya mkutano huu ni kutoa Taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kipindi cha nusu mwaka cha utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2019/2020

UJUMBE WA ASKOFU BANGONZA KWA WANAOOMBA BANK YA DUNIA KUINYIMA MIKOPO SERIKALI


Askofu Dk. Benson k. Bagonza

HEKIMA, UMOJA NA AMANI HIZI NI NGAO ZETU

''Serikali ikaomba mkopo Benki ya Dunia,

Huyu kaandika barua Benki ya Dunia kulalamika na kushauri mkopo usitolewe,

Mwingine akakemea na kuhukumu kuwa wanaoandika na kusema wanaichafua nchi. 

Hili ni somo kamili la URAIA darasa la saba, Civics kidato cha tatu, history paper two kidato cha tano.

Kwamba:

1. Kuna tofauti kati ya nchi na serikali. Ziko nchi zisizo na serikali, ziko nchi zina serikali mbili hata tatu, na serikali huja na kupita. Nchi hubaki.

2. Kuna tofauti kati ya Rais na serikali. Kuna nchi zina rais lakini hazina serikali; kuna nchi zina kitu kinaitwa serikali lakini hazina Rais. Kwa hiyo waweza kumkosoa Rais lakini usiikosoe serikali. Waweza kuikosoa serikali lakini usimkosoe Rais.

3. Mungu wetu ni mkarimu sana. Ameumba watu na kuwapa hata utashi wa kumkataa yeye aliyewaumba. Hata kwa nchi moja, wapo watu mbalimbali:

Kuna watu wanaweza kuipenda nchi wasiipende serikali. 

Kuna watu wanaweza kuipenda serikali wasimpende rais. 

Kuna watu wanaweza kumpenda rais wasiipende nchi. 

Kuna watu wanaweza kukipenda chama tawala wasiipende serikali.

Kuna watu wanaweza kumpenda rais wasikipende chama chake.

Kuna watu wanaweza kukipenda chama wasimpende kiongozi wake.

Kuna watu wanapenda niandikayo lakini wananichukia mimi!

Kuna watu wananipenda mimi lakini wanachukia niandikayo!

Hali kadhalika, kuna wanasiasa wengi wanapenda kura zetu lakini hawapendi mambo yetu.

Ndiyo maana jukumu kuu la kiongozi ni kuwaleta watu pamoja, kuwafanya kuvumiliana. Hakuna kazi ya hatari niijuayo kama ya kuwafanya watu wafikiri kwa njia moja, wafanane wanachopenda na kuchukia na kuwa na mtazamo mmoja kuhusu nchi na serikali yake. 

Daima tukumbuke, Kila penye mitume 12, Yuda Iskariote lazima awepo. Na U-Yuda daima umo ndani si nje. Bila Yuda, utume wa kundi lile ungekuwa mgumu.

Mwisho wa siku, bora aliyeandika kuliko wanaofikiri kama yeye na hawaandiki na wamo ndani ya serikali.'' Askofu Dk. Benson k. Bagonza

UTALII WAONGEZA MAPATO, TANZANIA IPO NAFASI YA NNE AFRIKA




SERIKALI imesema sekta ya utalii nchini imepiga hatua kubwa baada ya kushinda nafasi ya nne barani Afrika kwa kuingiza mapato mengi ya utalii ikitanguliwa na Afrika Kusini, Misri na Morocco.

Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk Hassan Abbas leo jijini Dodoma katika mkutano wake na wandishi wa habari uliolenga kutoa ufafanuzi katika mambo mbalimbali nchini ikiwemo Utalii, Uchumi na Elimu.

Dk Abbas amesema ripoti ya Taasisi maarufu za Utalii ya mwishoni wa mwaka jana, imeonesha kuwa kwa mwaka 2018 Tanzania  iliingiza Dola za Marekani Bilioni 2.43 kutoka Dola Bilioni 2.19 za mwaka 2017.

Amesema kwa miaka mitatu iliyopita mifumo ya kodi iliimarishwa huku baadhi ya watu wakatishia kuwa watalii watakimbia nchini, lakini wameongezeka zaidi na kuchangia kukua kwa uchumi.

" Shirika la utangazaji la kimataifa (CNN) katika taarifa ya Novemba, 2019, inasema Tanzania imekua ni nchi ya kwanza kuwa na maeneo mazuri na yakuvutia na kutembelea kuliko nchi zote za afrika," Amesema Dk Abbas.

Kwa upande wa makusanyo ya mapato, Dk Abbas amesema moja ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kusimamia mifumo ya kimageuzi ambayo sasa imeanza kuleta mafanikio makubwa na ya kihistoria nchini.

Amesema kwa miaka mitatu sasa habari kubwa katika mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano katika ukusanyaji wa mapato kwa mwezi ilikuwa ni kutoka Sh.Bilioni 850 mwaka 2015 hadi Sh.Trilioni 1.3.

“ Leo ninayo furaha kulitangazia rasmi Taifa kuwa kutokana na juhudi kubwa zilifanywa na Serikali kupitia TRA na Idara nyingine za Serikali, wastani wa mapato ya kodi kwa mwezi kati ya Julai-Disemba, 2019, umepanda na sasa ni sh. Trilioni 1.5 kwa mwezi na kuna mwezi tuliwahi kukusanya hadi Trilioni 1.7," Amesema Dk Abbas.

Akizungumzia sekta ya madini madini hasa mauzo ya nje ya madini taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania  (BOT) ya  Novemba, 2019, Takwimu zinaonesha kuwa mauzo ya bidhaa zisizo kuwa zile za kawaida yameongezeka kwa asilimia 31.0 kwa sababu kubwa mbili muhimu:

Moja alitaja kuwa ni Kuongezeka kwa mauzo ya dhahabu kwani  Serikali imechukua hatua  ya  kuanzisha masoko ya madini na kuzuia uuzaji holela na utoroshaji wa madini.

 Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma leo.



Wandishi mbalimbali wa vyombo vya habari wakifuatilia mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali uliofanyika ofisini kwake leo jijini Dodoma.



Msemaji Mkuu wa Serikali Dk Hassan Abbas akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na wandishi wa habari uliofanyika leo ofisini kwake jijini Dodoma

BASHUNGWA AMETOA WIKI MOJA KWA WAWEKEZAJI WALIOSHINDWA KUENDELEZA VIWANDA

BASHUNGWA AMETOA WIKI MOJA KWA WAWEKEZAJI WALIOSHINDWA KUENDELEZA VIWANDA

Waziri wa Viwanda na Biashara  Mhe. Innocent Bashungwa amewapa wiki moja wawekezaji wa kiwanda cha karatasi cha Mufundi Paper hills kufika ofisini kwake Mkoani Dodoma.

 Akizungumza katika ziara yake katika kiwanda hicho kilichopo mkoani Iringa, Mhe, Bashungwa ameshangwa na jinsi wawekezaji hao walivyoshindwa kukiendeleza kiwanda hicho.

Mhe. Bashungwa alisema kiwanda hakionyeshi kama kinakwenda na dhumuni la kuanzishwa kwake hapa nchini.
“Mwalimu Nyerere na Mhe. Rais John Pombe Magufuli sera zao ni sawa za kuendeleza viwanda nchini, lakini hapa sioni kama jambo hilo litafikiwa.

“Kiwanda hiki kilijengwa kwa gharama ya dola 260 milioni na kilipobinafsishwa kiliuzwa dola 26 milioni kwa wawekezaji ikiwa ni pungufu ya asilimia 90 ya thamani yake ya awali.
Mhe.Bashungwa alisema fedha hizo dola 26milioni hazikuingia Serikalini alipewa mwekezaji wa lengo la kufanyia ukarabati kiwanda ili kiweze kufanya kazi kwa ufanisi.

“Hadi sasa sijui kama hata kodi mnalipa kwa serikali, natoa wiki moja nataka uje Dodoma kwa ajili ya kulizungumza suala hili.
Mhe. Bashungwa aliongeza sema kiwanda hiki kilitengezwa kwa ajili ya kuondoa tatizo la upatikanaji wa karatasi nchini.

Mhe.Bashungwa alisema masuala ya usalama ya taifa yanamambo mengi hata hili linaweza kuwa iwapo mataifa mengine yakikataa tuuzia karatasi itakuwa ni tatizo kubwa.

“Watu watatushangaa tunashindwa kutengeza hata karatasi kwa ajili ya watoto wetu waliopo shuleni.

Kwa uapande wake muwekezaji katika kiwanda hicho alisema kiwanda kinashindwa kuzalisha karatasi nyeupe kutokana uhaba wa malighafi zinazozalisha bidhaa hiyo,hivyo alimuhaidi Mhe. Waziri kuzalisha karatasi hizo watakapotatua changamoto hiyo.

Kiwanda hicho kinazalisha takribani tani 52,000 ambazo huuzwa ndani nchi na katika nchi za afrika mashariki.









Eliud Rwechungura

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WA KARAGWE WAPEWA ELIMU YA BIASHARA NA KUTAMBUA FURSA SHERIA ZA KUFANYA BIASHARA MIPAKANI

    Taasisi ya Mama Alaska Jamii kwa kushirikiana na Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Trade Mark East Africa, Halmashau...