Akofu Benson Bagoza wa kanisa la KKKT Dayosisi ya karagwe
Waumini wa Kanisa la Kiinjili kirutheli Dayosisi ya Karagwe wameshiriki katika ibada ya kuliombea Taifa na katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Covid-19 {CORONA} katika ibada iliyofanyika leo iliyofanika katika kanisa la KKKT - Lukajange.
Na Jackius Joackim - Radio karagwe.
Ibada hiyo imeongozwa na Askofu wa kanisa hilo Dk. Benson K. Bagonza katika kanisa kuu la lukajange dayosisi ya Karagwe ambayo imekua maalumu kwa kuliombea Taifa na Dunia kwa ujumla katika maambukizi ya virus vya CORONA ambavyo vimekua tishio kwa nchi mbalimbali na dunia kwa ujumla
Askofu Bagonza ameendelea kusema kuwa wanadamu wamependa vitu vingine kuliko kumupenda Mwenyezi Mungu na kumupenda shethani kuliko Mwenyezi Mungu na kusema kuwa dunia imetenda dhambi kwa ujumla
Baadhi ya wachungaji walioshiriki katika ibada hiyo wamesema kuwa ni muda maalumu wa kuliombea Taifa katika ugojwa huu na kusema kuwa waumini na Wananchi kwa ujumla kufuata utaratibu unaotolwe na Serikali na wataalam wa afya
No comments:
Post a Comment
Kwa mawasiliano;
Eliud Rwechungura
0759646339
eliudrwechungura98@gmail.com
Karagwetv@gmail.com
Endelea kutufatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii
instagram: karagwetv
Facebook:karagwetv