SERIKALI IMETANGAZA UKOMO WA KIWANGO CHA JUU CHA BEI YA SUKARI KWA REJA REJA KWA KILA MKOA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Kulia) na Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa (Kushoto) wakizungumza na waandishi wa habari Wakati wakitoa taarifa kwa  umma wa Watanzania wote kuhusiana na Hali ya sukari nchini na mwenendo wa bei yake  katika msimu huu wa uzalishaji wa sukari wa 2019/2020. Jijini Dodoma, leo tarehe 23 Aprili 2020.
Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa (Kushoto )akisisitiza wafanyabiashara kote nchi kuzingatia kikomo cha bei ya sukari iliyotolewa na Serikali kwa wafanyabiashara wa reja reja kila mkoa Wakati wakitoa taarifa kwa  umma wa Watanzania wote kuhusiana na Hali ya sukari nchini na mwenendo wa bei yake  katika msimu huu wa uzalishaji wa sukari wa 2019/2020, {katikati} Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga, {kulia} Naibu waziri kilimo Mhe Omary Mgumba. Jijini Dodoma, leo tarehe 23 Aprili 2020.


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Katikati) akitangaza kikomo cha kiwango cha juu cha bei ya sukari kwa reja reja kwa kila mkoa Wakati wakitoa taarifa kwa  umma wa Watanzania wote kuhusiana na Hali ya sukari nchini na mwenendo wa bei yake  katika msimu huu wa uzalishaji wa sukari wa 2019/2020 {kushoto} Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa, {Kulia} Naibu waziri kilimo Mhe Omary Mgumba . Jijini Dodoma, leo tarehe 23 Aprili 2020.

**************************
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga na Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa wamekutana na waandishi wa habari ili kuzungumza  na umma wa Watanzania wote kuhusiana na Hali ya sukari nchini na mwenendo wa bei yake  katika msimu huu wa uzalishaji wa sukari wa 2019/2020.


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameanza kwa kueleza mahitaji na matumizi ya sukari nnchi ‘‘Mahitaji ya sukari ya matumizi ya kawaida Nchini yanakadiriwa kufikia tani 470,000 kwa Mwaka. Kiasi hiki ni kwa wastani wa mahitaji ya kiasi cha tani 38,000 kwa kila Mwezi pamoja na kiasi cha tani 14,000 kwa ajili ya dharura. 
Uwezo wa viwanda vyetu vya ndani kwa msimu wa 2019/20 kwa mujibu wa makadirio ya mwanzoni mwa msimu yaani Julai, 2019 ni kuzalisha takribani tani 378,000 za sukari. Kiasi hiki ni sawa na asilimia 82.9 ya mahitaji halisi ya tani 456,000 ambayo hayajumuishi kiasi cha dharura cha tani 14,000. 
Uwezo huu wa uzalishaji wa viwanda vya ndani unaacha pengo la kiasi cha tani 78,000 ili kuweza kutosheleza mahitaji halisi ya tani 456,000 bila kiasi cha dharura cha tani 14,000.
Hata hivyo, uwezo huu wa uzalishaji wa viwanda vya ndani ulitarajiwa kufikiwa pale tu panapokuwa na hali nzuri ya hewa na ufanisi mzuri wa viwanda’’


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameendelea kwa changamoto ambazo zimekumba msimu wa uzalishaji sukari wa Mwaka 2019/2020
‘‘Kutokana na ukweli kwamba msimu wa uzalishaji sukari wa Mwaka 2019/20 umekumbwa na changamoto kadha wa kadha zikiwemo 
Mvua nyingi kupita kiasi ambayo imepelekea uvunaji wa miwa kuwa mgumu,
Mlipuko wa magonjwa ya miwa kama vile viding’ata wa njano n.k,
Uharibifu wa mitambo ya baadhi ya viwanda na kuchelewa kupatiwa vipuri.
Sababu hizo zote kwa pamoja zimechangia kwa kiasi kikubwa Viwanda vyetu vya ndani kushindwa kufikia malengo ya kuzalisha tani 378,000 za sukari kwa msimu wa 2019/20.’’


Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa ametoa hali ya uzalishaji wa viwanda vya sukari nchini:
‘‘Kutokana na hali halisi ya uzalishaji wa ndani wa sukari kuwa pungufu ya malengo ya uzalishaji, Serikali ilifanya makadirio ya kiasi cha sukari ya kuziba pengo la uzalishaji (gap sugar) na kutoa vibali kwa wazalishaji ili kuweza kuagiza na kuingiza sukari hiyo Nchini kwa wakati kwa ajili ya kukidhi mahitaji. Hadi hivi sasa tunazungumza na nyinyi, sukari iliyoagizwa kuja kuziba pengo la uzalishaji takribani tani 10,710 imeshaingia nchini na inaendelea  kusambazwa katika Mikoa yote.
Mnamo tarehe 24, 28 na 30 Aprili, 2020 tunategemea kupokea jumla ya tani 13,500 za sukari ya kuziba pengo na tutaendelea kupokea kiasi kingine cha sukari Mwanzoni mwa Mwezi Mei, 2020. Kiasi chote cha sukari kilichopo Nchini na tunachoendelea kupokea kinatosheleza kabisa mahitaji ya sukari nchini. Kwa taarifa hii, tuwaombe Wananchi wote kuwa watulivu kwa sababu Nchi yetu inayo sukari ya kutosha.’’


Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa amesema serikali haitakubali kuona wafanyabiashara kupandisha bei kiholela
‘‘Tunapenda kuwatangazia Wafanyabiashara wote Nchini wenye tabia hizi za kupandisha bei kiholela waache mara moja kwani Serikali haipo tayari kuona Wananchi wake wanaumia kwa manufaa ya watu wachache. 
Serikali itachukua hatua kali kwa Mfanyabiashara yeyote ambaye atabainika kujinufaisha kwa kuuza sukari bei ya juu kulikoni bei ya kawaida ya soko.’’


Aitha, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga kabla ya kutangaza bei ya sukari ya reja reja Katika Mikoa yote nchini amesema;
Kwa mujibu wa Sheria ya Sukari  Na. 26 ya Mwaka 2001(Cap. 251) chini ya kifungu cha 11A inampa Mamlaka Waziri mwenye dhamana ya Kilimo kutangaza bei ya ukomo wa juu ya sukari.
Kutokana na changamoto ya wafanyabiashara kupandisha kiholela bei ya sukari nchini, Serikali tumeamua kuutangazia Umma wa Watanzania bei Kikomo ya sukari katika Mikoa yote Nchini Tanzania. Bei hizi kikomo zinalenga kukabaliana na changamoto ya kupanda kiholela kwa Bei ya Sukari Nchini ambayo kwa sasa imefikia wastani wa Shilingi 4,000/= hadi 4,500/= kwa kilo. Bei hii kikomo ya sukari imepangwa kwa kuzingatia gharama zote za uagizaji wa sukari ya kuziba pengo zinazotumiwa na wazalishaji kuagiza sukari kutoka nje ya Nchi.
Hivyo, kwa niaba ya Serikali tunapenda kuutangazia umma wa Watanzania kuwa bei ya sukari ya reja reja Katika Mikoa yote nchini itakuwa kama ifuatavyo;

KIWANGO CHA JUU CHA BEI YA SUKARI KWA REJA REJA KWA KILA MKOA 

NA.
MKOA
BEI YA  KILO (Tsh)






IRINGA 
2,900


MBEYA 
3,000


RUKWA 
3,200


KATAVI
3,200


RUVUMA 
3,200


NJOMBE
2,900


LINDI
2,800


MTWARA
2,800


ARUSHA
2,700


KILIMANJARO
2,700


MANYARA
2,700


TANGA 
2,700


DAR ES SALAAM
2,600


PWANI
2,700


MOROGORO
2,700


KAGERA
3,000


MWANZA
2,900


SIMIYU
2,900


SHINYANGA
2,900


GEITA
2,900


MARA
3,000


KIGOMA
3,200


SINGIDA
2,900


TABORA
2,900


DODOMA 
2,900


SONGWE
3,000






Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amemaliza kwa kusisitiza kuwa;
‘‘Bei hizi za ukomo za sukari zimezingatia umbali wa kila eneo katika Mikoa yote nchini. Niwaombe Wafanyabiashara wote nchini kuzingatia maelekezo haya ya Serikali. Yeyote atakayekiuka maelekezo haya atakuwa ametenda kosa na hivyo atafikishwa katika vyombo vya sheria ili apate adhabu ambayo itahusisha ama kunyang’anywa leseni ya biashara, kulipa faini au adhabu zote kwa pamoja. Tutachukua hatua kali za kisheria kwa mfanyabiashara yeyote ambaye atakiuka masharti haya.’’


Na Eliud Rwechungura – Wizara ya viwanda na biashara

IBADA ZA WASABATO ZIMEZINGATIA TAHADHALI ZA KUJIKINGA NA CORONA, WAUMINI WA WAMEITIKIA WITO WA RAIS WA KULIOMBEA TAIFA

          
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Aprili 18, 2020 ambapo ameshiriki katika ibada ambayo waumini hao wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.
Baadhi ya Wazee wa Kanisa wa Kanisa la SDA Bariadi mjini wakiwaongoza waumini wa kanisa hilo katika maombi maalum ya kuliombea Taifa, yaliyofanyika katika ibada Aprili 18, 2020 kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.(mwenye Tai wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka).
Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini wakiimba katika ibada ya Aprili 18, 2020 ambayo waumini wa kanisa hilo pia wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Marco Mlingwa akiwaongoza waumini wa kanisa hilo(hawapo pichani) katika maombi maalum ya kuliombea Taifa, yaliyofanyika katika ibada Aprili 18, 2020 kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.(wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka).
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Aprili 18, 2020 wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambapo ameshiriki ibada ambayo waumini hao wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.

Mmoja wa waimbaji wa kwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini akipuliza dawa katika vipaza sauti kuchukua tahadhari dhidi  ya maambukizi ya virusi vya Corona, kwenye ibada ambayo waumini wa Kanisa hilo wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.

********************************
Mchungaji wa Kanisa la SDA Bariadi Mjini, Marco Mlingwa amesema Kanisa hilo limepokea maelekezo ya Serikali na linaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuliombea Taifa Mungu aliponye na janga la Corona.

Kwa upande wao waumini wa Kanisa la SDA Bariadi Mjini wamemshukuru Mhe. Rais kuruhusu ibada kufanyika kwa kuzingatia maelekezo ya watalaam wa afya na kubainisha kuwa wataendelea kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Corona wakiamini kuwa Mungu atasikia wakiomba kwa imani na kwa bidii.

“Tunamshukuru Mhe. Rais kuruhusu ibada kuendelea kufanyika huku tukichukua tahadhari,  sisi Wakristo tunaamini watu tukiomba kwa bidii Mungu anasikia maombi, hivyo tukikutana na kuomba kwa bidii Mungu atasikia na kutuokoa na ugonjwa huu wa COVID 19,” alisema Paul Jidayi muumini SDA na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa.

“Sisi kama Wasabato tuna vipindi vyetu vya afya na kupitia vipindi hivyo tumeshajifunza na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona kanisani na majumbani; pia tunaungana na Rais kuliombea Taifa tukiamini kuwa Mungu atatusikia maana hata zamani, nchi ya Ninawi walipelekewa taarifa kuwa wataangamizwa lakini walipomlilia Mungu aliwasikia na  hawakuangamia,” alisema Mariam Manyangu.

KATIBU MKUU KILIMO AKERWA TFRA KUWA NA IDADI KUBWA YA WATENDAJI WANAOKAIMU


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Musabila Kusaya akiongea na Watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) pembeni yake kulia ni Mtendaji Mkuu wa TFRA, Dkt. Stephan Ngailo
Watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Bwana Gerald Musabila Kusaya wakati alipombela Makao Makuu ya Taasisi hiyo katika Ofisi za Jengo la Kilimo I, Temeke, Jijini Dar es Salaam

Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Kilimo pamoja na Watumishi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Bwana Gerald Musabila Kusaya wakati alipombela Makao Makuu ya Taasisi hiyo katika Ofisi za Jengo la Kilimo I, Temeke, Jijini Dar es Salaam
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) Dkt. Stephani Ngailo alikitoa neon la shukran mara baada ya Katibu Mkuu Bwana Gerald Musabila Kusaya kumaliza ziara ya kuitembelea TFRA katika ukumbi wa mikutano wa Kilimo I, Jijini Dar es Salaam

******************************

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Kusaya ameonyesha waziwazi kukerwa na Watendaji wengi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA) kukaimu kwenye nafasi zao na kutoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Kilimo kushirikiana na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Udhibiti Mbolea Tanzania ili kushughulikia kero hiyo.

Katibu Mkuu Bwana Gerald Kusaya amesema kwa kipindi kifupi ambacho amekuwa Wizara ya Kilimo, amekutana na changamoto ya Watendaji wengi kukaimu katika nafasi zao na kuongeza kuwa; hafuraishwi kuona jambo hilo likiendelea na kusisitiza kuwa sasa ni muda muhafaka wa kumaliza changamoto hiyo.

Baada ya kuapishwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli siku iliyofuata, nilikuja ofisini, Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi nilishuhudia Watendaji wengi, wakijitambulisha kuwa Makaimu; kukaimu si jambo geni na ni sehemu ya mchakato wa kumpata Kiongozi bora lakini unakuta Mtendaji anakaimu zaidi ya miezi sita (6) na wengine mpaka miaka mitatu (3) hii si sawa. Amesisitiza Katibu Mkuu.
“Napenda mfahamu kuwa, Sekta ya Kilimo inategemea nguvu kazi ya Watendaji wanaojiamini na wenye matumaini, sasa ukiwa na Mtendaji ambaye, anakaimu kwa muda mrefu ni vigumu kujituma na kuwa mbunifu kwa sababu hiyo inakuwa ngumu kuleta tija kwenye Taasisi nyeti kama Wizara yetu ya Kilimo. Amesisitiza Katibu Mkuu.

Katibu Mkuu Bwana Gerald Kusaya ameongeza kuwa haoni sababu kwa nini Mtendaji athibitishwi ili aongoze kama uwezo, sifa na vigezo anavyo na kuagiza kushughulikiwa mara moja kero hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa TFRA, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Kilimo na wa TFRA jambo hili lipo ndani ya uwezo wenu, litatueni haraka na kama kuna mahali mtakwama, nipo na mnifahamishe haraka iwezekanavyo; binafsi sipendi kuongoza Watendaji wanaokamimu si Wizarani Makao Makuu lakini pia hadi kwenye Taasisi za Wizara kama TRFA. Amemalizia Katibu Mkuu.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bwana Gerald Musabila Kusaya yupo kwenye ziara ya kuzitembelea Taasisi za Wizara ya Kilimo kwa lengo la kujitambulisha na kuwafaham Watumishi wa Taasisi ambapo leo (Jana) alitembelea Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea (TFRA), Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Kanda ya Kipawa, Bodi ya Chai pamoja na Wakala wa Wakulima Wadogo wa Chai (TSHTIDA). Taasisi zote hizi zipo Jijini, Dar es Salaam.
Kesho atazitembelea Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Mfuko wa Taifa wa Pemebejo za Kilimo (AGITF), Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Makao Makuu. Taasisi zote hizi zipo Jijini, Dodoma.

KAMPUNI YA EXPORT TRADING GROUP, YATOA MCHANGO WA CODID-19


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya  Sh. 500,000,000/= kutoka kwa Kampuni ya Export Trading Group,  ukiwa ni mchango wa Kampuni hiyo kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. Kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano, Frank Mtui, Kiongozi wa Kampuni (Tanzania) Niladri Choudhury, Afisa Uhusiano, Fatma Ally.  ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na uongozi wa Kampuni ya Export Trading Group, baada ya kupokea hundi ya  Sh. 500,000,000/= ,  ikiwa ni mchango wa Kampuni hiyo kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Aprili 14, 2020. Kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano, Fatma Ally, Afisa Uhusiano, Frank Mtui na Kiongozi wa Kampuni (Tanzania) Niladri Choudhury.  ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea hundi ya mfano ya sh. milioni 500 kutoka kampuni ya Export Trading Group (ETG) zikiwa ni msaada kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa homa ya mapafu unaotokana na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19) nchini.

Waziri Mkuu amepokea msaada huo leo (Jumanne, Aprili 14, 2020) ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma, kutoka kwa Mkurugenzi mkazi wa ETG, Bw. Nilladri Chowdhury aliyefuatana na maafisa uhusiano wa kampuni hiyo, Bw. Frank Mtui na Bi. Fatma Salum Ally.

Akizungumza mara baada ya kupokea kupokea msaada huo, Waziri Mkuu amewashukuru watendaji wa kampuni ya ETG kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya virusi vya corona, ambapo hadi sasa kesi 49 zimeripotiwa tangu kuanza kwa ugonjwa huo nchini na wagonjwa saba wameshapona.

“Kwa niaba ya Rais wetu, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tunawashukuru kwa msaada huu ambao utaisadia Serikali kupunguza makali ya kuwahudumia wananchi wetu. Tunahitaji kuungwa mkono na wadau wengine kama ninyi,” amesema.

Waziri Mkuu amewataka wananchi wote wazidishe kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo hasa katika kipindi hiki. “Hatua tuliyofikia hivi sasa, maambukizi yameanza kuongezeka hasa kwa Dar es Salaam na Zanzibar. Tunajua kule kuna watu wengi na shughuli zote za kiuchumi zinaanzia pale, lakini hatuna budi kufuata masharti tuliyopewa ili kuzuia ugonjwa huu usisambae,” amesema.

“Serikali inatoa msisitizo kwa wananchi wazingatie maelekezo yanayotolewa kuhusu kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona ikiwemo kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka pamoja na kujiepusha na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima.”

“Muhimu zaidi sote tuendelee kumuomba Mwenyezi Mkungu ili atupunguzie makali ya ugonjwa huu,” amesisitiza.

Mapema, akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kampuni ya ETG, Bw. Mahesh Patel, Mkurugenzi Mkazi wa ETG, Bw. Nilladri Chowdhury alisema wameamua kuchangia ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika vita ya kupambana na ugonjwa huo.

“Mwenyekiti wetu amesafiri lakini kama kampuni, tumeamua kuungana na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu, na ametutuma tutoe mchango wa shilingi milioni 500. Tuna imani na tunaendelea kumuomba Mungu ili atuvushe katika kipindi hiki,” alisema.

Alisema kampuni yao inashughulika na masuala ya kilimo zikiwemo kusambaza pembejeo na kuongeza thamani mazao kupitia kampuni yao ya Kapunga iliyoko Mbeya, viwanda vitatu vya kubangua korosho vilivyoko Mtwara, Newala na Tunduru na viwanda vya kusindika mbegu za mafuta.


Pia wanatoa soko kwa wakulima kwa kununua mazao kama vile korosho, mbaazi, kokoa, mahindi, choroko na ufuta.

WAZIRI MKUU, KASSIM MAJALIWA, AKUTANA NA KAMATI YA KITAIFA YA URATIBU WA MAPAMBANO DHIDI YA UGONJWA WA HOMA KALI YA MAPAFU (COVID - 19)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020.  ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020.  ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid, akizungumza jambo, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020.  ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akizungumza jambo, kwenye kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID - 19), kilichofanyika katika, ukumbi wa Hazina, jijini Dodoma, Aprili 14, 2020.  ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


VIFAA VYA KUPAMBANA NA CORONA VYAGAWIWA SONGWE


Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akipokea vitakasa mikono kutoka kwa Balozi wa Kampeni ya Mikono Safi, Tanzania Salama Mrisho Mpoto ambapo Wizara ya Afya imetoa vitakasa mikono lita 150 kwa Mkoa wa Songwe.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akipokea vitakasa mikono kutoka kwa Balozi wa Kampeni ya Mikono Safi, Tanzania Salama Mrisho Mpoto ambapo Wizara ya Afya imetoa vitakasa mikono lita 150 kwa Mkoa wa Songwe.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akinawa mikono kwa kutumia mashine ya kunawia bila kushika koki ambapo Wizara ya Afya imetoa mashine hizo mbili  kwa Mkoa wa Songwe, moja itawekwa katika Mpaka wa Tunduma na moja itawekwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila akinawa mikono kwa kutumia mashine ya kunawia bila kushika koki ambapo Wizara ya Afya imetoa mashine hizo mbili kwa Mkoa wa Songwe, moja itawekwa katika Mpaka wa Tunduma na moja itawekwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe George Kyando akinawa mikono kwa kutumia mashine ya kunawia bila kushika koki ambapo Wizara ya Afya imetoa mashine hizo mbili kwa Mkoa wa Songwe, moja itawekwa katika Mpaka wa Tunduma na moja itawekwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Kutoka Kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Kafulila, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe George Kyando, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela na na Mkuu wa Kitengo cha Maji Salama na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya Anyitike Mwakitalima wakionyesha mikono baada ya kunawa mapema leo.


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa vifaa mbalimbali vya kupambana na ugonjwa wa Virusi vya Corona kwa Mkoa wa Songwe huku ikiridhishwa na namna ambavyo Mkoa umechukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.
Hayo yamebainishwa mapema leo na Mkuu wa Kitengo cha Maji Salama na Usafi wa Mazingira kutoka Wizara ya Afya Anyitike Mwakitalima wakati akikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe vitakasa mikono lita 150, mashine za kutolea vitakasa mikono 30 na mashine mbili za kunawia bila kushika koki.
Mwakitalima amesema Wizara ya Afya inaendesha Kampeni ya Mikono Safi, Tanzania Salama ambapo pamoja na kutoa vifaa vya kupambana na ugonjwa wa virusi vya Corona kama vile vitakasa mikono pia hutoa elimu kwa wananchi namna ya kujikinga na Corona hasa kwa Mikoa iliyoko Mipakani kama Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ameipongeza Wizara ya Afya kwa kutoa vifaa hivyo hasa kwa Mkoa wa Songwe ambao upo Mpakani na ni Lango la kuingilia nchi za SADC ambapo vitakasa mikono 50 vinapelekwa katika jeshi la Polisi na 100 katika halmashauri zote.
Brig. Jen. Mwangela amesema,“Sisi Songwe ni Lango la SADC tukizubaa, tusipotoa elimu vizuri kwa Wananchi, tusipo chukua tahadhari ya kutosha tunaweza kuingiza Ugonjwa kutoka nchi jirani ambazo nazo zimeahirika na Corona”.
Ameongeza kuwa mpaka kufikia jana jumla ya wasafiri 180 wamewekwa karantini katika Halmashauri za Tunduma na Ileje  kwa muda wa siku 14 ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa Corona ambapo pia hakuna mshukiwa wa ugonjwa huo kwa Mkoa wa Songwe hadi sasa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe George Kyando ameishukuru Wizara ya Afya kwa kutoa kipaumbele kwa Jeshi hilo kwa kuwapatia vitakasa mikono kwakuwa wamekua wakisahaulika na wadau wengine huku akieleza kuwa anaendelea kutoa elimu kwa askari wachukue tahadhari zote muhimu wawapo katika majukumu yao.
Amesema katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Corona Jeshi la Polisi lina mchango mkubwa katika kulinda karantini na maeneo waliyotengwa wagonjwa wa Corona, pia kukagua mabasi na magari yote ya abiria hivyo wako katika hatari ya kuambukizwa.
Balozi wa Kampeni ya Mikono Safi, Tanzania Salama Mrisho Mpoto maarufu kama Mjomba amesema vita ya kupambana na Ugonjwa wa Virusi vya Corona inahitaji ushirikiano wa wananchi wote waweze kunawa kwa maji tiririka na sabuni kila wakati bila kuchoka na kutoona kama adhabu.
Mpoto amesema wananchi wa Songwe wanapaswa kuacha mila za kusalimiana kwa kushikana mikono, kukumbatiana, kubusiana kuepuka misongamano isiyo ya lazima kwa kuwa mafanikio yatapatikana kwa umoja ikiwa wananchi wote watazingatia kauli mbiu ya Jilinde na Umlinde Mwenzio.

SHULE ZOTE NA VYUO KUENDELEA KUFUNGWA – MAJALIWA, Sherehe za Muungano, Mei Mosi zaahirishwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema agizo la kufungwa kwa shule za awali, msingi, sekondari na vyuo vyote vya elimu ya kati na vya elimu ya juu litaendelea kubaki vile vile hadi hapo Serikali itakapotoa tamko jingine.

Pia, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. John Pombe Magufuli amesitisha maadhimisho ya Sherehe za Muungano (Aprili 26) pamoja na Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ili kuepuka msongamano na kuendelea kuzuia virusi vya corona visisambae zaidi. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 14, 2020) katika kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Mapambano Dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Mapafu unaotokana na maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID-19). Amesema hadi leo, nchini kuna jumla ya watu 53 waliobainika kuwa na virusi vya corona ikiwa ni ongezeko la wagonjwa wanne ambao wote wapo jijini Dar es Salaam.

Amesema Serikali bado haijatangaza kuhusu kufunguliwa kwa shule, vyuo na shughuli za michezo pamoja na misongamano isiyokuwa ya lazima, hivyo maeneo hayo yataendelea kusalia katika karantini na wanafunzi wote wandelee kubakia majumbani kwao.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli ameagiza sh. milioni 500 ambazo zilitengwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 56 ya Sherehe za Muungano zipelekwe kwenye mfuko wa kupambana na COVID-19 wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Pia, Waziri Mkuu amewaomba wadau mbalimbali waendelee kuiunga mkono Serikali katika mapambano dhidi ya virusi vya corona kwani janga hilo ni kubwa na wanaweza kutuma fedha kupitia akaunti Na: 9921159801 yenye jina la National Relief Fund Electronic.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema elimu ya tahadhari ni muhimu ikaendelea kutolewa kwa wananchi ili waweze kujikinga na maambukizi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona. “Kama si lazima kutoka, wananchi waendelee kutulia majumbani mwao.”

Amesema Wakuu wa Mikoa na Wilaya waendelee kusimamia utoaji wa elimu ya kujikinga na virusi hivyo hasa katika mkoa wa Dar es Salaam ambao unaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi ikifuatiwa na Zanziba. “Ni muhimu wananchi wake wakapewa tahadhari juu ya namna ya kijikinga.”

Waziri Mkuu ameagiza kuwa wataalamu wanaosimamia utoaji wa huduma katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wa watu wenye maambukizi ya COVID-19, wakiwemo madaktari wote wapewe vifaa vya kijikinga ili kuhakikisha hawapati maambukizi ya ugonjwa huo.

Amesema watu waliokutana na wagonjwa waendelee kufuatiliwa kwa umakini na wahusika wawashirikishe viongozi wote hadi wa ngazi za chini na kwamba athari za kiuchumi zinazojitokeza kufuatia ugonjwa huo ziendelee kuchambuliwa.

Machi 17, 2020 na Machi 18, 2020, Serikali ilitangaza kuzifunga shule za awali, msingi, sekondari na vyuo vyote vya elimu ya kati na vya elimu ya juu kwa muda wa siku 30 na kwamba wanafuzi wa kidato cha sita waliopaswa kuanza mitihani Mei 4, 2020 nao wangepaswa kusubiri Wizara ifanye utaratibu mwingine kulingana na matokeo ya hali ya maambukizi.

Akitangaza uamuzi huo, Waziri Mkuu pia alisisitiza kuwa mikusanyiko yote mikubwa ya ndani na nje isiyo ya lazima imesitishwa ikiwemo shughuli za michezo, matamasha ya muziki, mikutano mbalimbali ikiwemo ya shughuli za kisiasa, mahafali na shughuli nyingine za kijamii. 

Alizitaka wizara na taasisi zizitishe semina, warsha, makongamano na mikutano yote hapa nchini ambayo inahusisha washiriki toka nchi zenye maambukizi makubwa. “Watanzania wenye safari zisizo za lazima kwenye nchi zenye maambukizi makubwa, wanashauriwa wasitishe safari hizo,” alisisitiza.

Akielezea hatua nyingine zilizochukuliwa na Serikali ili kudhibiti ugonjwa huo, Waziri Mkuu alisema Serikali imesitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu ikiwemo Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL), Ligi Daraja la Pili (SDL) na aina nyngine.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 - DODOMA,                      
JUMANNE, APRIL 14, 2020.

ASKOFU BAGONZA WA KKKT - DAYOSISI YA KARAGWE AMEONGOZA IBADA YA KULIOMBEA TAIFA KWA MAPAMBANO YA CORONA

Akofu Benson Bagoza wa kanisa la KKKT Dayosisi ya karagwe
Waumini wa Kanisa la Kiinjili kirutheli Dayosisi ya Karagwe wameshiriki katika ibada ya  kuliombea Taifa na katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya  maambukizi ya virusi vya  Covid-19 {CORONA} katika ibada iliyofanyika leo iliyofanika katika kanisa la KKKT - Lukajange.

Na Jackius  Joackim - Radio karagwe.

Ibada hiyo imeongozwa na Askofu  wa kanisa hilo Dk. Benson K. Bagonza katika kanisa kuu la lukajange dayosisi ya Karagwe ambayo imekua maalumu kwa kuliombea Taifa na Dunia kwa ujumla katika maambukizi ya virus vya CORONA ambavyo vimekua tishio kwa nchi mbalimbali na dunia kwa ujumla

Askofu Bagonza ameendelea kusema kuwa wanadamu wamependa vitu vingine kuliko kumupenda Mwenyezi Mungu na kumupenda shethani kuliko Mwenyezi Mungu na kusema kuwa dunia imetenda dhambi kwa ujumla

Baadhi ya wachungaji walioshiriki katika ibada hiyo wamesema kuwa ni muda maalumu wa kuliombea Taifa katika ugojwa huu na kusema kuwa waumini na Wananchi kwa ujumla kufuata utaratibu unaotolwe na Serikali na wataalam wa afya

Hata hivyo Askofu amemaliza kwa kusema kuwa Wananchi wachukue tahadhali na ugojwa huu ambao umekua tishio kwa nchi nyingi hapa duniani na kusema kuwa dunia imetenda dhambi hivyo ni muda maalumu wa kutulia na kuliombea Taifa na nchi nyingine

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA NA WAZIRI WA KILIMO WAONGOZA KIKAO KAZI KUJADILI UFUNGAMANISHAJI WA SEKTA YA KILIMO NA MIKAKATI YA KUTAFUTA MASOKO


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Kushoto) na Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa (Kulia) wakifuatilia hoja za washiriki wa kikao kazi cha kujadili namna ya kufungamanisha uchumi wa Kilimo na Viwanda Jijini Dodoma, leo tarehe 1 Aprili 2020. 
(Picha Zote Na Eliud Rwechungura, Wizara ya Viwanda na Biashara)



Wataalamu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara kadhalika, Wizara ya Kilimo, na Taasisi za soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) na Taasisi ya kuendeleza Kilimo Afrika (AGRA) wamekutana Jijini Dodoma kujadili kwa pamoja namna ambavyo Wizara hizo mbili zinaweza kuongeza mshikamano na weledi wa kiutendaji kwa ajili ya kufungamanisha uchumi wa Kilimo na Viwanda.

Katika kikao hicho kilichotuama katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo maarufu kama Kilimo IV kikiongoza na mawaziri kutoka pande mbili, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) na Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa (Mb) kwa pamoja wamesisitiza ulazima wa wataalamu hao kuunganisha nguvu kwa pamoja baina ya Wizara na Taasisi za umma na binafsi ili kuimarisha upatikanaji wa takwimu sahihi kuhusu Uzalishaji, uhifadhi, Ubora kwa Mazao ya kimkakati na mchanganyiko.


Akizungumza katika kikao hicho Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa (Mb) amesema kuwa intelijensia ya masoko inapaswa kuhakikisha kwa haraka inatumia Balozi za Tanzania nje ya nchi katika kutafuta fursa za masoko ya Mazao  na bidhaa pamoja na kuanzisha madawati ya biashara (Trade/Commercial attache) Kwenye balozi hizo.


Pia amesema mpango mkakati wa kuwaunganisha wakulima na wasindikaji ndani na nje ya nchi ni muhimu kutekeleza haraka iwezekanavyo ikiwa ni pamoja na kujenga uwezo zaidi katika kuongeza Uzalishaji wenye tija ili kukidhi nahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.  



Kadhalika Waziri Bashungwa ameongeza kuwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) wanapaswa kukutana na Shirika la Chakula Duniani (WFP) kujadili uimarishaji wa masoko ya Mazao mbalimbali.


Naye, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet hasunga (Mb) amewataka Wataalamu hao kuimarisha intelijensia ya masoko kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo na ufuatiliaji wa karibu wa mwenendo wa masoko ya Mazao na bidhaa ulimwenguni.

Hasunga amesema kuwa  pamoja na mikakati ya masoko lakini wataalamu hao wanaweza kujadili na kuona namna ya kuimarisha uhifadhi wa Mazao ya wakulima baada ya kuvuna kwani Barani Afrika nafaka myingi hupotea mara baada ya kuvuna.


Amewataka wataalamu hao pamoja na mambo mengine amewataka kuhakikisha kuwa wanaimarisha miundombinu ya masoko ikiwemo maghala ya kisasa ya kuhifadhia Mazao na bidhaa.


Pamoja na mambo mengine Waziri Bashungwa ameitaka Taasisi ya kuendeleza Kilimo Barani Afrika (AGRA) kushirikiana na wadau wengine wa sekta ya Kilimo ili kutafuta ufunguzi wa namna ya kuimarisha masoko ya Mazao ya wakulima nchini.


































Na Eliud Rwechungra, Wizara ya Wizara ya Viwanda na Biashara-Dodoma 


MWISHO.

Eliud Rwechungura

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WA KARAGWE WAPEWA ELIMU YA BIASHARA NA KUTAMBUA FURSA SHERIA ZA KUFANYA BIASHARA MIPAKANI

    Taasisi ya Mama Alaska Jamii kwa kushirikiana na Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Trade Mark East Africa, Halmashau...