WAZIRI BASHUNGWA AMETOA MAAGIZO MAPYA YA KUPAMBANA NA CORONA


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ametoa maagizo ya kupiga marufuku ya uuzaji wa Ethanol nje ya nchi. 

maagizo hayo ameyatoa leo 27 mach,2020 ambapo ni siku mbili baada ya kufanya kikao kilichowakutanisha wazalishaji wa malighafi zinazotumika kutengeneza vitaka mikono { Hand sanitizer}

Hatua hii inalenga kuimalisha upatikanaji wa malighafi hiyo nchini ili kuviwezesha viwanda vya ndani kuzalisha kwa wingi vitakasa mikono na hii itasaidia kukabiliana na mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo nchini.

Aidha, Mheshimiwa Waziri amewataka wenye viwanda vinavyozalisha Ethanol kuongeza uzalishajiili kuhakikisha Ethanol inapatikana kwa wepesi hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inapambana na ugojwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona {COVID - 19}

Zuio hilo limeaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 27 machi,2020 




No comments:

Post a Comment

Kwa mawasiliano;
Eliud Rwechungura
0759646339
eliudrwechungura98@gmail.com
Karagwetv@gmail.com

Endelea kutufatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii
instagram: karagwetv
Facebook:karagwetv

Eliud Rwechungura

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WA KARAGWE WAPEWA ELIMU YA BIASHARA NA KUTAMBUA FURSA SHERIA ZA KUFANYA BIASHARA MIPAKANI

    Taasisi ya Mama Alaska Jamii kwa kushirikiana na Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Trade Mark East Africa, Halmashau...