KIFO CHA KWANZA CHA MTANZANIA MWENYE UGOJWA WA CORONA

“Kifo cha kwanza cha mgonwa wa COVIN-19 . Kimetokea leo machi 31, 2020, marehemu alikiwa Mtanzania mwenye umri wa miaka 49, ambaye pia alikuwa anasumbuliwa na maradhi mengi" Amesema Ummy Mwalimu Waziri wa Afya.


Waziri wa Viwanda na Biashara ampongeza mjasiriamali mtanzania aliyebuni kifaa maalumu cha kunawia mikono ili kujikinga na virusi vya Corona.





Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) leo tarehe 30 Machi, 2020 amepokea kifaa maalumu cha kunawia mikono kilichotengenezwa na mjasiriamali wa kitanzania ndugu. Jonas Urio (Ambaye anatokea katika mkoa wa Manyara).

Mhe. Bashungwa amempongeza sana ndugu Jonas Urio kwa ubunifu wake huu wa kutengeza kifaa kizuri na bora cha kunawia mikono ambacho kinaweza kutumiwa na
taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kuhudumia watu mbalimbali kusafisha mikono yao ili kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Mjasiriamali ndugu Jonas Urio ambaye ni mbunifu wa teknolojia hii ameishukuru Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kumpa ushirikiano tangu awali alipoanza ubunifu wake hadi kufikia hatua hii ambapo ameshasajiliwa na ubunifu wake utambulika.

Ndugu Jonas amesema, “Napokea ushauri wa maboresho ya klifaa hiki niliyopewa na Mhe Waziri na Naibu waziri ambao wote kwa pamoja wamefurahia sana ubunifu wangu, naahidi kufanyia kazi maboresho yote haraka ili kifaa hiki kingie sokoni ili kusaidia wananchi kujisafisha mikono na kupambana na ugonjwa huu wa Corona”


Na:
Eliud Rwechungura

WAZIRI BASHUNGWA AMETOA MAAGIZO MAPYA YA KUPAMBANA NA CORONA


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa ametoa maagizo ya kupiga marufuku ya uuzaji wa Ethanol nje ya nchi. 

maagizo hayo ameyatoa leo 27 mach,2020 ambapo ni siku mbili baada ya kufanya kikao kilichowakutanisha wazalishaji wa malighafi zinazotumika kutengeneza vitaka mikono { Hand sanitizer}

Hatua hii inalenga kuimalisha upatikanaji wa malighafi hiyo nchini ili kuviwezesha viwanda vya ndani kuzalisha kwa wingi vitakasa mikono na hii itasaidia kukabiliana na mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo nchini.

Aidha, Mheshimiwa Waziri amewataka wenye viwanda vinavyozalisha Ethanol kuongeza uzalishajiili kuhakikisha Ethanol inapatikana kwa wepesi hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inapambana na ugojwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona {COVID - 19}

Zuio hilo limeaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 27 machi,2020 




TAMKO LA JPM KUHUSU UCHAGUZI 2020



Uchaguzi tutafanya tu, wapo wengine wanadhani nitaahirisha nani anayetaka akae kwenye maofisi haya miaka yote hiy amesema Rais John Magufuli leo akipokea ripoti ya CAG na ya TAKUKURU.
“Hatujazuiliwa kukutana kisa corona, tunaendelea kukutana hata Nchi zilizoathirika na corona imeua Watu bado Mabunge yao yanaendelea,kazi lazima iendelee kufanyika na Uchaguzi tutafanya tu,wengine wanafikiri nitaahirisha, nani anataka akae kwenye Maofisi haya muda wote huo!?”-JPM

WAZIRI UMMY MWALIMU AMETOA RIPOTI MPYA YA UGOJWA WA CORONA

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema idadi ya wagonjwa wa Corona nchini imefikia kumi na tatu{13}, nane kati yao ni Watanzania na watano ni raia wa kigeni.Wagojwa nane wapo Dar es salaaam,Wagojwa wawili wapo Arusha,Wagojwa wawili wapo Zanzibar,Mgojwa mmoja yupo Kagera,
Wagojwa kumi na mbili wamesafiri nje ya Nchi na mmoja hakusafiri nje.




GSM IMEONDOA NGUVU YAKE YANGA SC















Kampuni ya GSM ambayo ni sehemu ya wadhamini wa Yanga SC imeiandikia barua club hiyo na kueleza kuwa imesitisha huduma zote ilizokuwa inazitoa kwa club hiyo nje ya mkataba wao kwa sababu ya kutuhumiwa kuwa inapora madaraka viongozi wa Yanga.





WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AMEWAKUTANISHA WAZALISHAJI WA MALIGHAFI ZINAZOTUMIKA KUTENGENEZA VITAKASA MIKONO (HAND SANITIZER)

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amefanya kikao na wamiliki na wasimamizi wa Viwanda vinavyotengeneza malighafi ya kutengeneza vitakasa mikono ( Hand Sanitizer).

Lengo la kikao hicho ilikuwa ni kujadiliana na wenye viwanda, wazalishaji pamoja na wadau wengine watakavyoweza kuongeza uzalishaji ili kufanikisha upatikanaji wa vifaa kwa ajiri ya kujikinga na usambaaji wa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona (COVID19).



Katika kikao hicho Kampuni la Kilombero Sugar imetoa lita 30,000 za alcohol bure kwa serikali zitaakazosaidia kutengeneza vitakasa mikono (Hand sanitizer) ili kusaidia juhudi za serikali za kupambana na virusi vinavyosababisha ugojwa wa Corona.


Pia kampuni ya Consumer Choice Ltd imetoa kwa serikali kiasi cha lita 10,000 za ethanol na pia imeamua kubadili matumizi ya Ethanol ambayo yalipaswa kutengeneza vilevi ambapo asilimia 75% za Ethanol zitatengeneza vitakasa mikono (hand sanitizer) na 25% ya Ethanol itakayobaki itatumika kutengeneza vilevi.


Kampuni ya Mount Meru Millers imetoa lita 10,000 ya Vitakasa mikono (Hand sanitizer) itakayosambazwa kwa vituo vya afya na taasisi nchini.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) amewataka wenye viwanda kuongeza uzalishaji wa malighafi za kutengeneza vitakasa mikono pia amewaelekeza TBS na FCC kuendelea kukagua wafanyabiashara wa vitakasa mikono ambao wanauza bidhaa feki na hafifu pia kwa wote wanaopandisha bei kwa lengo la kujinufaisha kuwachukulia hatua kali za kisheria kwani wanahatarisha maisha ya watanzania.



TAREHE 25 MACHI, 2020 UKUMBI WA LAPF DODOMA.

Eliud Rwechungura

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WA KARAGWE WAPEWA ELIMU YA BIASHARA NA KUTAMBUA FURSA SHERIA ZA KUFANYA BIASHARA MIPAKANI

    Taasisi ya Mama Alaska Jamii kwa kushirikiana na Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Trade Mark East Africa, Halmashau...