POLEPOLE, JIMBONI KWA BASHUNGWA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM

Ziara ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole jimboni Karagwe kwa shughuli za Ukaguzi wa Utekerezaji wa Ilani ya uchaguzi ikiwemo Ujenzi wa Majengo ya Chuo Cha Ufundi Karagwe (KDVTC), Ukaguzi wa majengo ya kituo cha afya Kayanga, Ukaguzi wa majengo na utendaji kazi wa Ofisi ya Uthibiti ubora wa Elimu wilaya karagwe na Mkutano wa kujumuika pamoja na kusherekea miaka minne ya ushindi wa uongozi wa awamu ya tano ya Rais Dr.John Pombe Mafuguli















NYAKAHANGA FC YATWAA UBINGWA WA BASHUNGWA KARAGWE CUP 2019


BASHUNGWA KARAGWE CUP 2019



Michuano ya Ligi ya Mbunge wa Jimbo la Karagwe Mh Innocent Ruga Bashungwa (Mb) ambae pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara imefikia tamati leo hii toka ilipoanza mwanzoni mwa mwezi Agost 2019 kwa timu ya Kata ya Nyakahanga kuchukua ubingwa huo katika msimu wa pili wa ligi hiyo, baada ya kuifunga timu ya Kata ya Kamagambo kwa penalti 3-2 Katika Uwanja mpya wa Bashungwa Stadium uliopo mjini Kayanga Wilayani Karagwe Mkoani Kagera.


Kilele cha mashindano hayo  kilitanguliwa na mchezo wa awali wa  mshindi wa tatu kwa kuzikutanisha Timu za kata ya Nyakabanga na Kayanga, ambapo Nyakabanga wameibuka kidedea kwa mikwaju ya penalti 4-2 dhidi ya Kata ya Kayanga baada ya Timu hizo kutoshana Nguvu kwa Dakika 90 za mchezo.

Mgeni rasmi katika mchezo wa Fainali hizo Mhe. Constantine Kanyasa (Mb) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii amesema amefurahishwa na Fainali hizo na huku akiduwazwa na umati wa mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo,  ikiwa ni ishara ya upendo mkubwa wa wananchi hao dhidi ya Mbunge wao pamoja na michezo kwa ujumla, licha ya mambo mengine Mhe. Kanyasu amesisiitiza juu ya Vijana na wananchi kuendelea kutangaza Utalii kupitia michezo hususani hifadhi mbili za Burigi - Chato na Ibanda - Rumanyika zilizopo katika Wilaya za Karagwe na Kyerwa.

Kwa upande wake Mwenyeji na muandaaji wa  mashindano hayo Mbunge wa jimbo la Karagwe Mh Innocent Luga Bashungwa, amewashukuru wote waliofanikisha mashindano hayo kubwa akizidi kumshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa namna ambavyo amekuwa akimsaidia kwa kumuunga mkono, lakini pia kwa jinsi alivyoendelea kumuamini na kwamba hatomuangusha 
Huku akiongeza kuwa kupitia michezo ataendeleza mshikamano na mahusiano kati ya Vijana na Serikali, ikiwa pia michezo ni ajira, afya na Utalii.

Bingwa wa michuano hiyo Timu ya Nyakahanga wameibuka na Kitita cha Shilingi  amejipatia Tsh 2,500, 000/=, jezi seti 1 na Kombe, 
Mshindi wa pili amejipatia Tsh 1,650,000/= na jezi seti 1.
Mshindi wa tatu amejipatia Tsh 450,000/= na jezi seti 1.
Mshindi wa nne amejipatia Tsh 300,000/ na jezi seti 1, huku Zawadi hizo zikinogeshwa na Zawadi kutoka Kwa Mgeni rasmi Aliyeongeza Laki mbili Kwa Mshindi wa kwanza na pili, wakati Mke wa Waziri Bashungwa Mama Alaska akiongeza Milioni Moja katika Zawadi za washindi .Zawadi nyingine ni Timu yenye nidhamu imejipatia jezi seti 1, Zawadi nyingine zilikuwa za: 
Golikipa bora, Mfungaji bora na Mchezaji bora kila mmoja amejinyakulia Tsh 50,000/=

Kupitia mashindano hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Jen. Marco Gaguti ametangaza mechi kati ya Bukoba combine na Karagwe Combine mchezo utakaochezwa wiki tatu zijazo na Mshindi atazawadiwa Milioni Mbili, na atakaeshindwa atapata kifuta jasho shilingi Milioni Moja.

Awali ligi hiyo ilishirikisha timu zote za kata  23 zilizopo Wilaya ya Karagwe huku kila timu ikipewa seti moja ya jezi na mpira mmoja kwa ajili ya michuano hiyo. Pia viongozi wengine waliohudhulia fainali hiyo ni Mkuu wa Wilaya Karagwe Mhe. Godfrey Mheluka viongozi  wa Chama na Serikali
na watu Mashuhuri.

 Photo by ELIUD RWECHUNGURA 0759646339
TIMU YA NYAKAHANGA IKIKABITHIWA KOMBE

MASHABIKI WA TIMU ZOTE

MASHABIKI WA TIMU ZOTE

WANAKARAGWE WAKITAZAMAZA MECHI

WANAKARAGWE WAKITAZAMAZA MECHI

KOMBE LIKILETWA UWANJANI

MCHEZO WA FAINALI UKIENDELEA

TIMU YA NYAKAHANGA IKIFANYA MABADILIKO

KOMBE LA LIGI

VIONGOZI WA LIGI
MCHEZO WA FAINALI UKIENDELEA

WANAKARAGWE WAKITAZAMAZA MECHI

WANAKARAGWE WAKITAZAMAZA MECHI

MH.WAZIRI AKITAZAMA MCHEZO KWA UMAKINI

MAMA ALASKA  MKE WA MH.BASHUNGWA AKITAZAMA MECHI YA FAINALI

MKUU WA MKOA, MGENI RASMI NA MH.BASHUGWA

VIONGOZI WA LIGI
SAID ABDALA MCHEZAJI WA KAYANGA BAADA YA KUKOSA PENALITI

TIMU YA KAMAGAMBO

TIMU YA NYAKAHANGA

WAAMUZI WA FAINALI

UTAMBULISHO WA WACHEZAJI

MGENIRASMI NA MH.BASHUNGWA 

JUMA MCHEZAJI WA TIMU YA KAYANGA

VIONGOZI KUTOKA OFISI YA WAZIRI NA MBUNGE



Eliud Rwechungura

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WA KARAGWE WAPEWA ELIMU YA BIASHARA NA KUTAMBUA FURSA SHERIA ZA KUFANYA BIASHARA MIPAKANI

    Taasisi ya Mama Alaska Jamii kwa kushirikiana na Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Trade Mark East Africa, Halmashau...