Timu ya kata ya Ihembe imeibuka mabingwa wa
Bashungwa Karagwe Cup 2017 baada ya kuifunga Nyaishozi mabao 2-1. Mchezo
huo uliopigwa katika uwanja wa Changarawe huku mgeni rasmi akiwa Waziri
wa Mambo ya ndani Mheshimiwa Mwigulu Nchemba uliteka hisia za mamia ya
wakazi wa jimbo la Karagwe waliojitokeza kwa wingi.
Ihembe walikuwa wa kwanza kupata goli dakika 25
kupitia kwa Athumani Chuji aliepiga shuti kali la mpira wa adhabu
uliomshinda golikipa wa Nyaishozi na kuingia wavuni. Bao hilo
lilionekana kuwachanganya Nyaishozi ambao walionyesha kutoelewana katika
eneo la ulinzi na kujikuta wakiruhusu bao la pili katika dakika ya 35
lililofungwa na Mshauri Kato aliewatoka walinzi wa Nyaishozi na kufunga
goli la kiustadi. Kipindi cha pili Nyaishozi waliuanza mchezo kwa kasi
na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 78 lililofungwa na
mshambuliaji MC, hata hivyo jitihada za kusawazisha matokeo
zilikwamishwa na mlinda mlango wa Ihembe alieokoa michomo mingi.
Kufuatia ushindi huo Ihembe walijipatia kombe na
kiasi cha fedha shilingi milioni moja na nusu huku Nyaishozi wakipata
shilingi laki saba na nusu kama kifuta jasho kwa kushika nafasi ya pili.
Akizungumza baada ya mchezo huo mbunge wa Karagwe Mheshimiwa Innocent
Bashungwa alisema mashindano hayo yatakuwa endelevu kila mwaka ili
kuibua vipaji vya vijana wa Karagwe waweze kujiajiri kupitia michezo na
kuahidi kuboresha mashindano yajayo kwa kusaka wadau wengine
watakaohakikisha wilaya ya Karagwe inakuwa na timu bora ya kushiriki
ligi kuu.
No comments:
Post a Comment
Kwa mawasiliano;
Eliud Rwechungura
0759646339
eliudrwechungura98@gmail.com
Karagwetv@gmail.com
Endelea kutufatilia kwenye mitandao yetu ya kijamii
instagram: karagwetv
Facebook:karagwetv