Mh.Innocent Bashungwa akizungumza na wanakikundi cha Kayanga Youth Morden Funitures.
Mh.Innocent Bashungwa akiwa na baadhi ya wanakikundi wa Kayanga Youth Morden Funitures.
Katibu wa mbunge Ndg. Ivvo Ndisanye akiwa na wakikundi cha Tuinuane mafundi katwe "TUMAKA"
Katibu wa mbunge Ndg. Ivvo Ndisanye akiwa na baadhi ya wanakikundi cha MVIKIKA.
Mradi wa ufugaji wa mbuzi wa mwakikundi katika kijiji cha katwe.
Mmoja wa wakikundi cha Tuinuane mafundi katwe "TUMAKA"
Mbunge wa wilaya ya Karagwe mh. Innocent Bashungwa amefanya ziara jimboni kwake ya kuvitembelea vikundi vyenye miradi mbalimbali vya maendeleo jimboni kwake ili kuweza kujua utendaji kazi wa vikundi hiyo pamoja na changamoto wanazoozipata katia vikundi hivyo.
Mheshimiwa mbunge ameanza kwa kuutembelea mradi wa kikundi cha vijana Seremala kiitwacho "KAYANGA YOUTH MORDEN FUNITURES" ambapo kikundi hicho kina jumla ya vijana tisa(9).
Kikundi hicho kinajihusisha na utenezaji wa samani za majumbani kama vile sofa,kabati,vitanda.
Mradi huo wa vijana upo mjini Kayanga - Karagwe ambao ulizinduliwa tarehe 03/08/2017 na Ndg. Amour Hamad Amour kiongozi wa mbio mwenge kitaifa.
Mwekititi wa kikundi hicho Timotheo Enock ameanza kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais pamoja na Halimashauri ya wilaya ya Karagwe kwa kukipa mkopo kikundi hicho Milioni nne (4,000,000) ili waweze kujikwamua katika janga la umasikini.
Wanakikundi hao wamepata nafasi ya kumueleza mbunge baadhi ya mafanikio ambayo amekwisha kuyapata ikiwa ni pamoja na kuweza kununua vifaa vya kuweza kutengeneza samani mbalimbali kwa wakati mmoja, sambamba na hayo wanakikundi hao wameiomba serikali iwawezeshe kwa kuwaongezea mkopo ili wapate kununua mashine za kisasa za kutengenezea samani zenye ubora.
Pamoja na hao Mheshimiwa Bahungwa amepata nafasi ya kuweza ya kuwaelimisha vijana hao jinsi ya kuboresha mradi wao na amewahaidi kuwafutia soko zuri la samani wanazozitengezeza katika kikundi chao
Pia ziara ya mbunge imendelea kwa kuvitembelea vikundi vingine ishirini na moja (21) vilivyopo vijiji cha Katwe,Katembe na Kituntu katika kata ya Kituntu wilaya ya Karagwe ambavyo ni Tuinuane mafundi katwe "TUMAKA" pamoja na na kikundi cha MVIKAKI kinachoongoza vikundi ishirini (20) ,vikundi hivyo vilianzishwa mwaka 2011
Mwekiti wa vikundi hivyo Bi.Masitura Jamada ameeleza mafanikio ya vikundi hivyo ikiwa ni pamoja na kuwajengea nyumba wanakikundi kumi, wanawafadhiri wanafunzi tisa katika elimu ya sekondari, wanatoa elimu kwa kwa wanakikundi ambao hawajui kusoma na kuandika pia kila kikundi wana miradi ya ufugaji wa ngombe, mbuzi na kuku .
by
Eliud Rwechungura
0759646339 / 0623206642
karagwe - kagera