PROF. SHEMDOE ‘‘TUWEKEZE KWENYE VIWANDA VINAVYOTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI’’


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe wa kwanza (kulia) akizungumza na  Mkurugenzi Kiwanda kuzalisha mafuta ya kupikia cha Bugili Investment Bw. Nkuba Bugili wa kwanza (kushoto) alipofanya ziara katika kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu. {Picha na Wizara ya Viwanda na Biashara}


 Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe wa kwanza (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa kiwanda cha Bugiri Investment Bw.Nkuba Bugiri alipokuwa anamueleza mambo mbalimbali kuhusu kiwanda hicho. Wa kwanza (kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Ludovick Nduhiye.


Sehemu ya mashine za kukamulia mafuta ya alizeti katika kiwanda cha Bugiri Investment kilichopo Wilaya ya Maswa Mkoa wa Shinyanga.


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe amewataka Watanzania kuwekeza katika sekta ya viwanda vinavyotumia malighafi za ndani.

Prof. Shemdoe aliyasema hayo Mkoani Simiyu alipokuwa katika ziara ya siku moja kutembelea Viwanda katika Mkoa huo. Katika ziara hiyo Katibu Mkuu na ujumbe wake walipata fursa ya kutembelea kiwanda kipya cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha cha Bugari Investment Ltd kinachomilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100.

Prof Shemdoe alisema Bw. Bugari ameonyesha umuhimu wa kuwa na malengo katika kutekeleza jambo lolote.

 “ukiwa na malengo unaweza kufanya kitu chochote, hivyo natoa rai kwa watanzania wengine ambao wanaweza kuiga mfano huu  kufika mahali hapa na kujifunza, maana yote yanawezekana ukiweka nia”.

Kiwanda cha Bugari Investment Ltd  kimejengwa kwa gharama ya Sh. bilioni 2  kinatarajiwa kutoa ajira kwa Watanzania 65 ikiwa ni  ajira za kudumu na za muda pamoja na kuchangia mapato kwa Serikali kupitia kodi mbalimbali.

Prof Shemdoe aliishukuru Serikali ya Mkoa kwa kumpa ushirikiano mwekezaji huyo na kumuwezesha kufanikisha kutimiza azma yake ya kujenga kiwanda. Pia alizishukuru Taasisi za fedha kwa kumuamini na kumpatia mkopo uliofanikisha kujenga kiwanda hicho.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Bw. Festo Kiswaga alisema wananchi wa Simiyu na mikoa ya jirani wamepata uhakika wa soko la alizeti kwa kuwepo kiwanda hicho.

“Tumekuwa tukiwasisitiza wananchi kulima, lakini changamoto iilikuwa upatikanaji wa masoko, hivyo uwepo wa kiwanda hiki utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Mkoa huu na mikoa jirani’’.

Aidha alitoa wito kwa wananchi wa bariadi kuendelea kuzalisha alizeti kwa wingi ili kiwanda kiendelee kupata malighafi ya kutosha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Nkuba Bugari alisema ujenzi wa kiwanda hicho umeanza mwaka 2015 na upo katika hatua za mwisho na ujenzi na kinatarajiwa kukamilika na kuanza uzalishaji mapema hivi karibuni.

Bugari alisema wazo la kujenga kiwanda hicho alipata  baada ya kupata hamasa kutoka kwa Mhe. Rais   Dkt. John Joseph Magufuli alipotoa rai kwa Watanzania kujenga viwanda.

“Ndugu Watanzania wezangu tusiache bahati hii ya kuwa na Mhe. Magufuli, ni kwa namna gani Mhe. Rais anajitoa kwa ajili watanzania katika kufanikisha Tanzania ya Viwanda”.

Anasema mashine zilizofungwa katika kiwanda hicho zina uwezo wa kuchakata mbegu za alizeti, pamba na karanga.

 Aliongeza kiwanda hicho kina uwezo wa kuchakata tani elfu arobaini na nane  za mbegu za alizeti. Hivyo lengo lao ni kushika soko la ndani pamoja kuuza mafuta hayo nje ya nchi ya Tanzania.Aidha aliwasisitiza watanzania kuwa na uthubutu katika kutimiza malengo mbalimbali.

BASHUNGWA AMEELEKEZA WAMILIKI WA VIWANDA NCHINI KUKATA BIMA ZA MOTO.

  Waziri wa viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa{aliyevaa koti} akiongea na uongozi wa kiwanda kukoboa kahawa cha Amri Amir AL-HABSSY kilichoungua kwa moto Mei 07, 2020 ambacho chanzo chake ni hitilafu ya umeme iliyotokana na radi kubwa iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo iliyosabisha hasara ya takribani Tsh.1,328,940,000.00 Karagwe, Kagera {Picha na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara}

 

Waziri wa viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa{aliyevaa koti} akikagua kiwanda kukoboa kahawa cha Amri Amir AL-HABSSY kilichoungua kwa moto Mei 07, 2020 ambacho chanzo chake ni hitilafu ya umeme iliyotokana na radi kubwa iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo iliyosabisha hasara ya takribani Tsh.1,328,940,000.00 kushoto ni mmilioki wa kiwanda Karim Amri, kulia ni Mkuu wa wilaya Karagwe Godfrey Muheruka. Karagwe, Kagera {Picha na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara}

Mashine za kiwanda cha kukoboa kahawa cha Amri Amir AL-HABSSY kilichoungua kwa moto Mei 07, 2020 ambacho chanzo chake ni hitilafu ya umeme iliyotokana na radi kubwa iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo iliyosabisha hasara ya takribani Tsh.1,328,940,000.00, Karagwe, Kagera


 


Waziri wa viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amewataka wamiliki wa viwanda nchini kuhakikisha wanakata bima za moto ili pale wanapokumbwa na ajali za moto wapate wepesi wa kulipwa fidia za mali zao.

 

Bashungwa alitoa wito huo akiwa ziarani Karagwe mkoani Kagera 17 mei 2020, baada ya kutembelea na kukagua kiwanda cha kukoboa kahawa cha Amri Amir AL-HABSSY kilichoungua kwa moto Mei 07, 2020 nakuona mashine zilivyoharibika baada ya kuunguzwa na moto ambao chanzo chake ni hitilafu ya umeme iliyotokana na radi kubwa iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo.

 

Akiongea baada ya kukagua Mhe. Bashungwa alitoa pole kwa mkurugenzi wa kiwanda hicho Karim Amri pamoja na wafanyakazi ambao kwasasa wamepoteza ajira zao, ambapo alirithishwa na hatua ambazo zimekwishachukuliwa na wamiliki wa kiwanda hicho ambazo ni kufatilia bima kwaajili ya kulipwa fidia.

 

“Tunapokuwa na viwanda hatujui mambo ya kesho na keshokutwa, mambo ya ajari unaweza kupanga kila kitu lakini hakuna anayetegemea ajari itatokea muda gani, kwahiyo kupitia kiwanda hiki nitoe wito kwa viwanda vyote nchini tuwe tunakata bima, maana kiwanda hiki kimeungua lakini walikuwa na bima ya moto.”

 

 

Awali  meneja wa kiwanda hicho Daniel Ndayanse akitoa taarifa kwa Waziri alieleza  hasara walioipata baada ya kufanya tathimini ya hasara iliyotokana na kuungua kwa kiwanda hicho kuwa ni mashine za kiwanda ni takribani Tsh.1,328,940,000.00 na jingo la takribani Tsh. 49,275,750.00 na kuongeza kuwa kiwanda kilikuwa na waajiliwa wa kudumu 16 ambao wapo kwa kipindi chote cha mwaka na wakati wa msimu huwa kinaajili watu kuanzia 800 hadi 1000 kulingana na kazi ya siku.

 

Aidha, Meneja alieleza kuwa “Kiwanda chetu tulikuwa tumekiimalisha kwa kukifanya cha kisasa ambapo tuliweza kuzalisha kati ya tani 50 hadi tani 65 za kahawa safi ambazo ni takribani gunia kati ya 800 hadi 1,000 kwa masaa 24, kwa kukoboa kahawa maganda kati ya tani 115 hadi tani 140 kwa masaa hayo 24 kama hakuna tatizo la umeme.”

 

Kwaupande wake mmiliki wa kiwanda Bw.Karim Amri alimshukuru Mhe.Rais John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuimarisha na kuweka sera bora za viwanda kwa wawekezaji nchini, ambapo alitumia fursa hiyo kutoa maombi maalumu kwa Mhe.Waziri Bashungwa.

 

“Tunakuomba wewe Mhe.Waziri kuweka msukumo kwa watu wa bima BRITAM INSURANCE ambao tulikata bima kwao waweze kutufanyia haraka watulipe ili tuweze kununua mashine kufikia mwezi julai mwaka huu kiwanda kianze kufanya kazi”.

 

Alisema kuwa pamoja na mafanikio waliyo nayo kwa upande wa viwanda wilayani Karagwe alifafanua changamoto kubwa inayowasumbu mara kwa mara kuwa ni tatizo la umeme ambalo limekuwa tatizo sugu kwa wenye viwanda ambapo alisema kuwa kuna siku umeme unakatika na kuwaka Zaidi ya mara 20 hivyo husababisha kuungua kwa Motors,taa, na mitambo mingine.

 

 

Kufatia kukithiri kwa matukio ya moto wilayani Karagwe, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake mkuu wa wilaya Godfrey Muheruka imeamua kujenga kituomcha zima moto na uokoaji ambacho kitakuwa kikisaidia kwenye ajali za moto pale zinapotokea.

 

 

Hata hivyo kitendo cha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya karagwe kuamua kujenga jingo la zima moto na uokoaji kikamshawishi waziri Bashungwa kuchangia mifuko 200 ya saruji na kuwataka wadau wa maendeleo kuchangia ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.

Eliud Rwechungura

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WA KARAGWE WAPEWA ELIMU YA BIASHARA NA KUTAMBUA FURSA SHERIA ZA KUFANYA BIASHARA MIPAKANI

    Taasisi ya Mama Alaska Jamii kwa kushirikiana na Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Trade Mark East Africa, Halmashau...