WANAWAKE WAJASIRIAMALI WA KARAGWE WAPEWA ELIMU YA BIASHARA NA KUTAMBUA FURSA SHERIA ZA KUFANYA BIASHARA MIPAKANI

 



 Taasisi ya Mama Alaska Jamii kwa kushirikiana na Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Trade Mark East Africa, Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Karagwe, wamezindua semina yenye lengo la kutoa elimu ya biashara, kutambua sheria za kufanya biashara mipakani na kuzitambua fursa mbalimbali za biashara kwa wanawake wajasiriamali wa wilaya Karagwe.

 

Semina hiyo imezinduliwa leo Mei 17, 2021 katika ukumbi wa Tripple P, Omurushaka Karagwe Kagera na itatolewa kwa kata zote 23 za wilaya ya Karagwe kwa kuwafikia wanawake wajasiriamali 300 ambao ni wawakilishi wa vikundi wanaotegemewa kupeleka elimu hii kwenye vikundi vyao ili kuwafikia wajasiriamali zaidi ya 4,000 wa Karagwe ili kuleta tija kwenye Biashara zao.

 


Wakati akifungua Semina hiyo, Afisa biashara mkoa wa Kagera, kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Bw. Issaya Tendegu amewataka wanawake wajasiriamali wa wilaya ya Karagwe kulima kilimo chenye tija kwa kutumia mbegu bora ambazo zinaongeza thamani ya mazao katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

 

Aidha, Bw. Issaya Tendegu amezitaja fursa nyingi za kibiashara zilizopo wilaya ya Karagwe na kutoa ufafanuzi wa fursa kubwa ya kijiografia ya Karagwe kuwa moja kati ya wilaya iliyopo mpakani mwa Tanzania na nchi nyingine za jirani kama Uganda, Rwanda na Burundi.

 


Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Mama Alaska Jamii, Bi. Jennifer Bashungwa, ameeleza semina itakavyowasaidia akina mama wajasiliamali kutambua na kufahamu sheria za kufanya biashara mipakani zitakazowasaidia kunufaika na soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kupitia semina hizi za biashara,  wanawake wajasiliamali wa wilaya ya karagwe watajengewa uwezo na uelewa wa kukuza biashara na kutambua fursa za masoko yaliyowazunguka.

 


Taasisi ya Mama Alaska Jamii imekua ikitoa mafunzo ya biashara kwa makundi mbalimbali ya wajasiliamali wakiwemo Mama Lishe wa Mkoa wa Dar es salaam na wakulima wa zao la mpunga wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

 

 


 

 

 

TIMU YA NYAISHOZI FC YAPOKEA UDHAMINI WA JEZI NA PESA KUTOKA KWA HLUCKY KOMBUCHA INV. DC MHERUKA AMEWAOMBA WANANCHI NA WADAU KUENDELEA KUICHANGIA TIMU.

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka (kulia) akipokea jezi kutoka Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha investment, Bw. Hamis Jumanne ambao ni wadhamini wa timu ya Nyaishozi FC mabingwa wa ligi mkoa Kagera wanaoenda kushiriki ligi ya mabigwa wa Mikoa (RCL2021) ambapo timu hiyo itachezea mechi katika kituo cha Katavi imepagwa kundi D, nyuma ni kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Karagwe Kagera, Leo, Machi 01, 2021.



Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka (kulia) akipokea kiasi cha pesa kutoka Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha investment, Bw. Hamis Jumanne ambao ni wadhamini wa timu ya Nyaishozi FC mabingwa wa ligi mkoa Kagera wanaoenda kushiriki ligi ya mabigwa wa Mikoa (RCL2021) ambapo timu hiyo itachezea mechi katika kituo cha Katavi imepagwa kundi D, nyuma ni kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Karagwe Kagera, Leo, Machi 01, 2021.


 


Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha investment, Bw. Hamis Jumanne akiwa katika picha pamoja na Katibu Msaidizi wa msaidizi wa Chama cha mpira mkoa Kagera, Majaliwa Said na Kocha Msaidizi wa timu ya Nyaishozi Fc, Jonson Majara mara baada ya kukabidhi jezi ya pesa za kusaidia timu ya Nyaishozi FC mabingwa wa ligi mkoa Kagera wanaoenda kushiriki ligi ya mabigwa wa Mikoa (RCL2021) ambapo timu hiyo itachezea mechi katika kituo cha Katavi imepagwa kundi D, Karagwe Kagera, Leo, Machi 01, 2021.



Na Eliud Rwechungua.



Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka amewaomba wadau na wananchi wa mkoa Kagera kuendelea kuichangia timu ya Nyaishozi FC ambao ni mabingwa wa ligi mkoa Kagera wanaoenda kushiriki ligi ya mabigwa wa Mikoa (RCL2021) ambapo timu hiyo imepagwa kundi D na itachezea mechi katika kituo cha Katavi.


Mheruka ameyasema leo, Machi 01, 2021 alipokuwa akipokea jezi za wachezaji na pesa ya kuisaidia timu kutoka kwa kambuni ya Hlucky Kombucha investment ambao ni wazalishaji wa kinywaji cha Kombucha Ginger Drink ambao ni wadhamini wa timu ya Nyaishizi FC.


‘‘Nitoe wito kwa Wananchi wote na wadau waendelee kuichangia timu yetu Nyaishozi, Timu hii imetutoa kimaso maso ni timu ambayo ni mabingwa wa ligi ya Mkoa wa Kagera lakini pia niwashukuru umoja wa Wanakaragwe wanaoishi Dar es salaam nao wanaendelea kufanya michango yao kupitia WhatsApp pia Jambo Bukoba ambao tumeshapokea michango yao”


Mheruka ameendelea kumpongeza Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha investment, Bw. Hamis Jumanne ambae amekuwa mstali wa mbele kwa kujitoa kuiwezesha timu hiyo pia kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya wilaya Karagwe pia  ameonekana akiandaa matamasha mbalimbali ya kutafuta na kuinua vipaji vya vijana ndani ya wilaya Karagwe.



Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni Hlucky Kombucha investment, Bw. Hamis Jumanne amesema kuwa Kampuni yake imeamua kuunga mkono timu ya Nyaishozi FC ili kuunga mkono michezo ndani ya mkoa lakini pia kuumunga mkono Rais wetu pia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa ambaye ndie Mbunge wa Jimbo la Karagwe kwa sababu tuna timu ambayo imewakilisha wilaya Karagwe vizuri na sasa inaendelea kuuwakilisha Mkoa vizuri katika ligi ya Mikoa (RCL2021)


Aidha, Bw. Hamis Jumanne ameendelea kuihakikishia timu ya Nyaishozi FC kuwa atakuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine kuunga mkoa timu hiyo ili iweze kushinda katika ligi ya mikoa ili hata wilaya ya Karagwe tupate hata timu ya Kutuwakilisha katika ligi Daraja la pili panapo majaliwa.


Naye, Kocha Msaidizi wa timu ya Nyaishozi Fc, Jonson Majara amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Karagwe na mkoa wa Kagera kuwa tayali timu ipo kambini na imeshajipanga vizuri kwa kushirikiana na benchi la ufundi na uongozi wa timu kuhakikisha inarudi na ushindi ili angalau mkoa upate timu ya pili inayocheza ligi katika daraja la juu, itapendeza sana kwasababu timu hii ni timu ya wanannchi ukizingatia namna ambavyo wanaendelea kujitoa kwa ajili ya timu hiyo.

 

Awali, Katibu Msaidizi wa msaidizi wa Chama cha mpira mkoa Kagera, Majaliwa Said amewashukuru wananchi na wadau wote wanaoendelea kujitoa na kuunga mkono timu ya Nyaishozi maana timu bado ni changa kushiriki ligi hizi na amehaidi atashirikiana na timu kuhakikisha inapata ushindi katika ligi hiyo inayoanza Machi 04, 2021 huko mkoani Katavi.


Mwisho.


IBADA SHUKRANI KUMBUKUMBU YA MWAKA MMOJA BAADA YA KIFO CHA MZEE NEKEMIA KAZIMOTO.




Picha ya Marehemu Nekemia Musa Kazimoto katika ibada ya shukrani iliyofanyika  leo tarehe 23 Disemba 2020 ikiwa ni mwama mmoja baada ya kutwaliwa kwake, alizaliwa mwaka 1937 katika kijiji cha Nyakahanga, Wilaya ya Karagwe, Mkoa Kagera na alifariki 19 Disemba 2019 na kuzikwa nyumbani kwake Kayanga, Karagwe tarehe 23 Disemba 2019.



Mchungaji Jovinali Karoro wa Kanisa la kiijiri la Kirutheli Tanzania KKKT usharika wa Kayanga akiongoza ibada ya shukrani ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kutwaliwa kwa Mzee Nekemia Musa Kazimoto, ibada hiyo imefanyika nyumbani kwake Omugakoroho, Kayanga Karagwe. Leo tarehe 23 Disemba 2020



Mama Florence Wamara, mke wa Nekemia kazimoto (katikati) akitoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa neema ambayo ameendelea kuijalia familia yake tangu kuondokewa na mzee wao, katika ibada ya shukrani ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kutwaliwa kwa Mzee Nekemia Musa Kazimoto, ibada hiyo imefanyika nyumbani kwake Omugakoroho, Kayanga Karagwe. Leo tarehe 23 Disemba 2020. Kulia ni Florence Kazimoto, Mtoto kwa kwanza wa Mzeee Nekemia, Kushoto ni Getrode Jacob.




Mzee Clement Nsherenguzi (kulia) aliyekuwa rafiki wa karibu Mzee Nekemia Kazimoto akiyaeleza  maisha halisi ya mzee Kazimoto katika ibada ya shukrani ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kutwaliwa kwa Mzee Nekemia Musa Kazimoto, ibada hiyo imefanyika nyumbani kwake Omugakoroho, Kayanga Karagwe. Leo tarehe 23 Disemba 2020. Kushoto ni Mama Florence Wamara, mke wa Nekemia kazimoto.


Familia ya Mzee Nekemia Kazimoto ikiwa katika kaburi ya Mzee Nekemia Kazimoto baada ya ibada ya shukrani ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kutwaliwa kwa Mzee Nekemia Musa Kazimoto, ibada hiyo imefanyika nyumbani kwake Omugakoroho, Kayanga Karagwe. Leo tarehe 23 Disemba 2020.



Na Eliud Rwechungura


Ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kuondokewa na Mzee Nekemia Musa Kazimoto, Leo tarehe 23 Disemba 2020 Familia ya Mzee Kazimoto imefanya ibada ya shukrani ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kumuombea mzee wao, ibada hiyo imefanyika nyumbani Omugakorongo, Karagwe, Kagera.


Nekemia Musa Kazimoto alizaliwa mwaka 1937 katika kijiji cha Nyakahanga, Wilaya ya Karagwe, Mkoa Kagera na alifariki Mwezi Disemba 2019 na kuzikwa nyumbani kwake Kayanga, Karagwe tarehe 23 Disemba 2019.


Mzee Kazimoto aliwahi kufanya kazi katika mashirika ya umma, Serikalini na vyama vya wafanyakazi hadi kuwa Rais wa Tanzania Federation of Labour (TFL), alikuwa mfanyabiashara aliyefanikiwa, mkulima na mfugaji bora. Pia, amewahi kuwa mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya Karagwe, taasisi na asasi za dini na zisizokuwa za Serikali. 


Mzee Nekemia Kazimoto aliwapa wosia wanaoukoo na wasomaji wake hasa watoto wake kumi na nne (Saba wa kike na saba wa kiume) na mke mmoja kwa kuandika kitabu cha hitoria yake kiitwacho "Maisha na Harakati za Kazimoto"


"Nawaomba sana mpokee wosia huu kwa wapenzi, kwani mimi nikiwa kama mwenzenu, mzazi, babu, rafiki, niite vyovyote upendavyo, nimebahatika kama wengine wengi, kuishi zaidi ya miaka sabini ulimwenguni hapa. Nimepata raha nyingi na shida za hapa na pale ikiwa ni sehemu ya maisha ya binadamu. Sijutii kwa lolote kwani nakubaliana na mafundisho ya dini yasemayo Mwenyezi Mungu ndiye muumba wetu, mpangaji na kiongozi wa maisha yetu, hivyo tumshukuru Kwa kila jambo" aliandika Mzee Nekemia Kazimoto katika kitabu cha Maisha na Harakati za Kazimoto.


Wakati akiongoza ibada shukrani Mchungaji wa Kanisa la KKKT wa usharika wa Kanyanga, Mch. Jovinali Karoro ameleza mambo mengi aliyoyafanya mzee Nekemia kazimoto huku akiwataka ndugu na jamaa kuyaishi mambo na matendo mema aliyoyafanya wakati wa uhai wake ambapo alikuwa mcha Mungu na Kiongozi katika Kanisa.


"Wapendwa leo tunahitimisha maombolezo na sasa tuna safari nyingine mpya kuanzia leo na safari hii ni hasa ya kuenzi mambo mazuri  ya mzazi wenu aliyojishughulisha nayo mpaka maisha yake alipokoma hapa duniani na nipande kutaja machache tu, jambo la kwanza alijivunia sana ukristo wake mpaka ametwaliwa alikuwa mkristo hai mwenye msimamo na imani yake, jambo la pili alijishughulisha sana na  na kutumia vizuri wakati wake katika kuzalisha bila kupoteza wakati, jambo la tatu alipenda sana  kudumisha umoja ndani na nje ya familia na kanisa pia, mzee huyu hakuwa na tabia ya kutangatanga" Anesema Mchungaji Karoro.


Nae Florence Wamara, mke wa Nekemia Kazimoto amepata nafasi katika ibada ya kutoa shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa neema ambayo ameendelea kuijalia familia yake tangu kuondokewa na mzee wao amezidi kutoa shukrani kwa ndugu, jamaa na majirani kwa kuendelea kuwa karibu na familia yao


"wana wa Mungu mliofika leo hapa tunawashukru sana mmetuonesha upendo wenu, siku ya msindikiza baba yetu mzee Kazimoto tuliona umati mkubwa kutoka pande zote kuja kuungana na kuomboleza nasi, hatujapata nafasi ya kumshukru kila mmoja ila itoshe kusema asanteni nyote kwa kila namna mlivyojitoa na Mungu wa Majeshi hatawapungukia" amesema mama Florence.


Kwa upande wake Mzee Clement Nsherenguzi aliyekuwa rafiki wa karibu amepata nafasi ya kuyaeleza maisha halisi ya mzee Kazimoto huku akieleza namna walivyoishi wote kwa upendo


"Mimi natoa shukrani zangu kwa Mungu kwa sababu niliondokewa na pacha wangu, Kazimoto nilikuwa namzidi mwaka mmoja lakini katika maisha yangu zaidi ya 90% ameniongoza na kunilea yeye maana tumejuana kwa miaka 75 tangu mwaka 1944 tukiwa watoto wadogo" Ameshema Mzee Nsherenguzi.



MWISHO


PROF. SHEMDOE ‘‘TUWEKEZE KWENYE VIWANDA VINAVYOTUMIA MALIGHAFI ZA NDANI’’


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe wa kwanza (kulia) akizungumza na  Mkurugenzi Kiwanda kuzalisha mafuta ya kupikia cha Bugili Investment Bw. Nkuba Bugili wa kwanza (kushoto) alipofanya ziara katika kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu. {Picha na Wizara ya Viwanda na Biashara}


 Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe wa kwanza (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa kiwanda cha Bugiri Investment Bw.Nkuba Bugiri alipokuwa anamueleza mambo mbalimbali kuhusu kiwanda hicho. Wa kwanza (kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Ludovick Nduhiye.


Sehemu ya mashine za kukamulia mafuta ya alizeti katika kiwanda cha Bugiri Investment kilichopo Wilaya ya Maswa Mkoa wa Shinyanga.


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe amewataka Watanzania kuwekeza katika sekta ya viwanda vinavyotumia malighafi za ndani.

Prof. Shemdoe aliyasema hayo Mkoani Simiyu alipokuwa katika ziara ya siku moja kutembelea Viwanda katika Mkoa huo. Katika ziara hiyo Katibu Mkuu na ujumbe wake walipata fursa ya kutembelea kiwanda kipya cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha cha Bugari Investment Ltd kinachomilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100.

Prof Shemdoe alisema Bw. Bugari ameonyesha umuhimu wa kuwa na malengo katika kutekeleza jambo lolote.

 “ukiwa na malengo unaweza kufanya kitu chochote, hivyo natoa rai kwa watanzania wengine ambao wanaweza kuiga mfano huu  kufika mahali hapa na kujifunza, maana yote yanawezekana ukiweka nia”.

Kiwanda cha Bugari Investment Ltd  kimejengwa kwa gharama ya Sh. bilioni 2  kinatarajiwa kutoa ajira kwa Watanzania 65 ikiwa ni  ajira za kudumu na za muda pamoja na kuchangia mapato kwa Serikali kupitia kodi mbalimbali.

Prof Shemdoe aliishukuru Serikali ya Mkoa kwa kumpa ushirikiano mwekezaji huyo na kumuwezesha kufanikisha kutimiza azma yake ya kujenga kiwanda. Pia alizishukuru Taasisi za fedha kwa kumuamini na kumpatia mkopo uliofanikisha kujenga kiwanda hicho.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Bw. Festo Kiswaga alisema wananchi wa Simiyu na mikoa ya jirani wamepata uhakika wa soko la alizeti kwa kuwepo kiwanda hicho.

“Tumekuwa tukiwasisitiza wananchi kulima, lakini changamoto iilikuwa upatikanaji wa masoko, hivyo uwepo wa kiwanda hiki utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Mkoa huu na mikoa jirani’’.

Aidha alitoa wito kwa wananchi wa bariadi kuendelea kuzalisha alizeti kwa wingi ili kiwanda kiendelee kupata malighafi ya kutosha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bw. Nkuba Bugari alisema ujenzi wa kiwanda hicho umeanza mwaka 2015 na upo katika hatua za mwisho na ujenzi na kinatarajiwa kukamilika na kuanza uzalishaji mapema hivi karibuni.

Bugari alisema wazo la kujenga kiwanda hicho alipata  baada ya kupata hamasa kutoka kwa Mhe. Rais   Dkt. John Joseph Magufuli alipotoa rai kwa Watanzania kujenga viwanda.

“Ndugu Watanzania wezangu tusiache bahati hii ya kuwa na Mhe. Magufuli, ni kwa namna gani Mhe. Rais anajitoa kwa ajili watanzania katika kufanikisha Tanzania ya Viwanda”.

Anasema mashine zilizofungwa katika kiwanda hicho zina uwezo wa kuchakata mbegu za alizeti, pamba na karanga.

 Aliongeza kiwanda hicho kina uwezo wa kuchakata tani elfu arobaini na nane  za mbegu za alizeti. Hivyo lengo lao ni kushika soko la ndani pamoja kuuza mafuta hayo nje ya nchi ya Tanzania.Aidha aliwasisitiza watanzania kuwa na uthubutu katika kutimiza malengo mbalimbali.

BASHUNGWA AMEELEKEZA WAMILIKI WA VIWANDA NCHINI KUKATA BIMA ZA MOTO.

  Waziri wa viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa{aliyevaa koti} akiongea na uongozi wa kiwanda kukoboa kahawa cha Amri Amir AL-HABSSY kilichoungua kwa moto Mei 07, 2020 ambacho chanzo chake ni hitilafu ya umeme iliyotokana na radi kubwa iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo iliyosabisha hasara ya takribani Tsh.1,328,940,000.00 Karagwe, Kagera {Picha na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara}

 

Waziri wa viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa{aliyevaa koti} akikagua kiwanda kukoboa kahawa cha Amri Amir AL-HABSSY kilichoungua kwa moto Mei 07, 2020 ambacho chanzo chake ni hitilafu ya umeme iliyotokana na radi kubwa iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo iliyosabisha hasara ya takribani Tsh.1,328,940,000.00 kushoto ni mmilioki wa kiwanda Karim Amri, kulia ni Mkuu wa wilaya Karagwe Godfrey Muheruka. Karagwe, Kagera {Picha na Eliud Rwechungura – Wizara ya Viwanda na Biashara}

Mashine za kiwanda cha kukoboa kahawa cha Amri Amir AL-HABSSY kilichoungua kwa moto Mei 07, 2020 ambacho chanzo chake ni hitilafu ya umeme iliyotokana na radi kubwa iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo iliyosabisha hasara ya takribani Tsh.1,328,940,000.00, Karagwe, Kagera


 


Waziri wa viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amewataka wamiliki wa viwanda nchini kuhakikisha wanakata bima za moto ili pale wanapokumbwa na ajali za moto wapate wepesi wa kulipwa fidia za mali zao.

 

Bashungwa alitoa wito huo akiwa ziarani Karagwe mkoani Kagera 17 mei 2020, baada ya kutembelea na kukagua kiwanda cha kukoboa kahawa cha Amri Amir AL-HABSSY kilichoungua kwa moto Mei 07, 2020 nakuona mashine zilivyoharibika baada ya kuunguzwa na moto ambao chanzo chake ni hitilafu ya umeme iliyotokana na radi kubwa iliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo.

 

Akiongea baada ya kukagua Mhe. Bashungwa alitoa pole kwa mkurugenzi wa kiwanda hicho Karim Amri pamoja na wafanyakazi ambao kwasasa wamepoteza ajira zao, ambapo alirithishwa na hatua ambazo zimekwishachukuliwa na wamiliki wa kiwanda hicho ambazo ni kufatilia bima kwaajili ya kulipwa fidia.

 

“Tunapokuwa na viwanda hatujui mambo ya kesho na keshokutwa, mambo ya ajari unaweza kupanga kila kitu lakini hakuna anayetegemea ajari itatokea muda gani, kwahiyo kupitia kiwanda hiki nitoe wito kwa viwanda vyote nchini tuwe tunakata bima, maana kiwanda hiki kimeungua lakini walikuwa na bima ya moto.”

 

 

Awali  meneja wa kiwanda hicho Daniel Ndayanse akitoa taarifa kwa Waziri alieleza  hasara walioipata baada ya kufanya tathimini ya hasara iliyotokana na kuungua kwa kiwanda hicho kuwa ni mashine za kiwanda ni takribani Tsh.1,328,940,000.00 na jingo la takribani Tsh. 49,275,750.00 na kuongeza kuwa kiwanda kilikuwa na waajiliwa wa kudumu 16 ambao wapo kwa kipindi chote cha mwaka na wakati wa msimu huwa kinaajili watu kuanzia 800 hadi 1000 kulingana na kazi ya siku.

 

Aidha, Meneja alieleza kuwa “Kiwanda chetu tulikuwa tumekiimalisha kwa kukifanya cha kisasa ambapo tuliweza kuzalisha kati ya tani 50 hadi tani 65 za kahawa safi ambazo ni takribani gunia kati ya 800 hadi 1,000 kwa masaa 24, kwa kukoboa kahawa maganda kati ya tani 115 hadi tani 140 kwa masaa hayo 24 kama hakuna tatizo la umeme.”

 

Kwaupande wake mmiliki wa kiwanda Bw.Karim Amri alimshukuru Mhe.Rais John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuimarisha na kuweka sera bora za viwanda kwa wawekezaji nchini, ambapo alitumia fursa hiyo kutoa maombi maalumu kwa Mhe.Waziri Bashungwa.

 

“Tunakuomba wewe Mhe.Waziri kuweka msukumo kwa watu wa bima BRITAM INSURANCE ambao tulikata bima kwao waweze kutufanyia haraka watulipe ili tuweze kununua mashine kufikia mwezi julai mwaka huu kiwanda kianze kufanya kazi”.

 

Alisema kuwa pamoja na mafanikio waliyo nayo kwa upande wa viwanda wilayani Karagwe alifafanua changamoto kubwa inayowasumbu mara kwa mara kuwa ni tatizo la umeme ambalo limekuwa tatizo sugu kwa wenye viwanda ambapo alisema kuwa kuna siku umeme unakatika na kuwaka Zaidi ya mara 20 hivyo husababisha kuungua kwa Motors,taa, na mitambo mingine.

 

 

Kufatia kukithiri kwa matukio ya moto wilayani Karagwe, kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake mkuu wa wilaya Godfrey Muheruka imeamua kujenga kituomcha zima moto na uokoaji ambacho kitakuwa kikisaidia kwenye ajali za moto pale zinapotokea.

 

 

Hata hivyo kitendo cha kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya karagwe kuamua kujenga jingo la zima moto na uokoaji kikamshawishi waziri Bashungwa kuchangia mifuko 200 ya saruji na kuwataka wadau wa maendeleo kuchangia ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati.

SERIKALI IMETANGAZA UKOMO WA KIWANGO CHA JUU CHA BEI YA SUKARI KWA REJA REJA KWA KILA MKOA

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Kulia) na Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa (Kushoto) wakizungumza na waandishi wa habari Wakati wakitoa taarifa kwa  umma wa Watanzania wote kuhusiana na Hali ya sukari nchini na mwenendo wa bei yake  katika msimu huu wa uzalishaji wa sukari wa 2019/2020. Jijini Dodoma, leo tarehe 23 Aprili 2020.
Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa (Kushoto )akisisitiza wafanyabiashara kote nchi kuzingatia kikomo cha bei ya sukari iliyotolewa na Serikali kwa wafanyabiashara wa reja reja kila mkoa Wakati wakitoa taarifa kwa  umma wa Watanzania wote kuhusiana na Hali ya sukari nchini na mwenendo wa bei yake  katika msimu huu wa uzalishaji wa sukari wa 2019/2020, {katikati} Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga, {kulia} Naibu waziri kilimo Mhe Omary Mgumba. Jijini Dodoma, leo tarehe 23 Aprili 2020.


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Katikati) akitangaza kikomo cha kiwango cha juu cha bei ya sukari kwa reja reja kwa kila mkoa Wakati wakitoa taarifa kwa  umma wa Watanzania wote kuhusiana na Hali ya sukari nchini na mwenendo wa bei yake  katika msimu huu wa uzalishaji wa sukari wa 2019/2020 {kushoto} Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa, {Kulia} Naibu waziri kilimo Mhe Omary Mgumba . Jijini Dodoma, leo tarehe 23 Aprili 2020.

**************************
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga na Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa wamekutana na waandishi wa habari ili kuzungumza  na umma wa Watanzania wote kuhusiana na Hali ya sukari nchini na mwenendo wa bei yake  katika msimu huu wa uzalishaji wa sukari wa 2019/2020.


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameanza kwa kueleza mahitaji na matumizi ya sukari nnchi ‘‘Mahitaji ya sukari ya matumizi ya kawaida Nchini yanakadiriwa kufikia tani 470,000 kwa Mwaka. Kiasi hiki ni kwa wastani wa mahitaji ya kiasi cha tani 38,000 kwa kila Mwezi pamoja na kiasi cha tani 14,000 kwa ajili ya dharura. 
Uwezo wa viwanda vyetu vya ndani kwa msimu wa 2019/20 kwa mujibu wa makadirio ya mwanzoni mwa msimu yaani Julai, 2019 ni kuzalisha takribani tani 378,000 za sukari. Kiasi hiki ni sawa na asilimia 82.9 ya mahitaji halisi ya tani 456,000 ambayo hayajumuishi kiasi cha dharura cha tani 14,000. 
Uwezo huu wa uzalishaji wa viwanda vya ndani unaacha pengo la kiasi cha tani 78,000 ili kuweza kutosheleza mahitaji halisi ya tani 456,000 bila kiasi cha dharura cha tani 14,000.
Hata hivyo, uwezo huu wa uzalishaji wa viwanda vya ndani ulitarajiwa kufikiwa pale tu panapokuwa na hali nzuri ya hewa na ufanisi mzuri wa viwanda’’


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameendelea kwa changamoto ambazo zimekumba msimu wa uzalishaji sukari wa Mwaka 2019/2020
‘‘Kutokana na ukweli kwamba msimu wa uzalishaji sukari wa Mwaka 2019/20 umekumbwa na changamoto kadha wa kadha zikiwemo 
Mvua nyingi kupita kiasi ambayo imepelekea uvunaji wa miwa kuwa mgumu,
Mlipuko wa magonjwa ya miwa kama vile viding’ata wa njano n.k,
Uharibifu wa mitambo ya baadhi ya viwanda na kuchelewa kupatiwa vipuri.
Sababu hizo zote kwa pamoja zimechangia kwa kiasi kikubwa Viwanda vyetu vya ndani kushindwa kufikia malengo ya kuzalisha tani 378,000 za sukari kwa msimu wa 2019/20.’’


Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa ametoa hali ya uzalishaji wa viwanda vya sukari nchini:
‘‘Kutokana na hali halisi ya uzalishaji wa ndani wa sukari kuwa pungufu ya malengo ya uzalishaji, Serikali ilifanya makadirio ya kiasi cha sukari ya kuziba pengo la uzalishaji (gap sugar) na kutoa vibali kwa wazalishaji ili kuweza kuagiza na kuingiza sukari hiyo Nchini kwa wakati kwa ajili ya kukidhi mahitaji. Hadi hivi sasa tunazungumza na nyinyi, sukari iliyoagizwa kuja kuziba pengo la uzalishaji takribani tani 10,710 imeshaingia nchini na inaendelea  kusambazwa katika Mikoa yote.
Mnamo tarehe 24, 28 na 30 Aprili, 2020 tunategemea kupokea jumla ya tani 13,500 za sukari ya kuziba pengo na tutaendelea kupokea kiasi kingine cha sukari Mwanzoni mwa Mwezi Mei, 2020. Kiasi chote cha sukari kilichopo Nchini na tunachoendelea kupokea kinatosheleza kabisa mahitaji ya sukari nchini. Kwa taarifa hii, tuwaombe Wananchi wote kuwa watulivu kwa sababu Nchi yetu inayo sukari ya kutosha.’’


Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa amesema serikali haitakubali kuona wafanyabiashara kupandisha bei kiholela
‘‘Tunapenda kuwatangazia Wafanyabiashara wote Nchini wenye tabia hizi za kupandisha bei kiholela waache mara moja kwani Serikali haipo tayari kuona Wananchi wake wanaumia kwa manufaa ya watu wachache. 
Serikali itachukua hatua kali kwa Mfanyabiashara yeyote ambaye atabainika kujinufaisha kwa kuuza sukari bei ya juu kulikoni bei ya kawaida ya soko.’’


Aitha, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga kabla ya kutangaza bei ya sukari ya reja reja Katika Mikoa yote nchini amesema;
Kwa mujibu wa Sheria ya Sukari  Na. 26 ya Mwaka 2001(Cap. 251) chini ya kifungu cha 11A inampa Mamlaka Waziri mwenye dhamana ya Kilimo kutangaza bei ya ukomo wa juu ya sukari.
Kutokana na changamoto ya wafanyabiashara kupandisha kiholela bei ya sukari nchini, Serikali tumeamua kuutangazia Umma wa Watanzania bei Kikomo ya sukari katika Mikoa yote Nchini Tanzania. Bei hizi kikomo zinalenga kukabaliana na changamoto ya kupanda kiholela kwa Bei ya Sukari Nchini ambayo kwa sasa imefikia wastani wa Shilingi 4,000/= hadi 4,500/= kwa kilo. Bei hii kikomo ya sukari imepangwa kwa kuzingatia gharama zote za uagizaji wa sukari ya kuziba pengo zinazotumiwa na wazalishaji kuagiza sukari kutoka nje ya Nchi.
Hivyo, kwa niaba ya Serikali tunapenda kuutangazia umma wa Watanzania kuwa bei ya sukari ya reja reja Katika Mikoa yote nchini itakuwa kama ifuatavyo;

KIWANGO CHA JUU CHA BEI YA SUKARI KWA REJA REJA KWA KILA MKOA 

NA.
MKOA
BEI YA  KILO (Tsh)






IRINGA 
2,900


MBEYA 
3,000


RUKWA 
3,200


KATAVI
3,200


RUVUMA 
3,200


NJOMBE
2,900


LINDI
2,800


MTWARA
2,800


ARUSHA
2,700


KILIMANJARO
2,700


MANYARA
2,700


TANGA 
2,700


DAR ES SALAAM
2,600


PWANI
2,700


MOROGORO
2,700


KAGERA
3,000


MWANZA
2,900


SIMIYU
2,900


SHINYANGA
2,900


GEITA
2,900


MARA
3,000


KIGOMA
3,200


SINGIDA
2,900


TABORA
2,900


DODOMA 
2,900


SONGWE
3,000






Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amemaliza kwa kusisitiza kuwa;
‘‘Bei hizi za ukomo za sukari zimezingatia umbali wa kila eneo katika Mikoa yote nchini. Niwaombe Wafanyabiashara wote nchini kuzingatia maelekezo haya ya Serikali. Yeyote atakayekiuka maelekezo haya atakuwa ametenda kosa na hivyo atafikishwa katika vyombo vya sheria ili apate adhabu ambayo itahusisha ama kunyang’anywa leseni ya biashara, kulipa faini au adhabu zote kwa pamoja. Tutachukua hatua kali za kisheria kwa mfanyabiashara yeyote ambaye atakiuka masharti haya.’’


Na Eliud Rwechungura – Wizara ya viwanda na biashara

IBADA ZA WASABATO ZIMEZINGATIA TAHADHALI ZA KUJIKINGA NA CORONA, WAUMINI WA WAMEITIKIA WITO WA RAIS WA KULIOMBEA TAIFA

          
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Aprili 18, 2020 ambapo ameshiriki katika ibada ambayo waumini hao wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.
Baadhi ya Wazee wa Kanisa wa Kanisa la SDA Bariadi mjini wakiwaongoza waumini wa kanisa hilo katika maombi maalum ya kuliombea Taifa, yaliyofanyika katika ibada Aprili 18, 2020 kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.(mwenye Tai wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka).
Kwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini wakiimba katika ibada ya Aprili 18, 2020 ambayo waumini wa kanisa hilo pia wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Marco Mlingwa akiwaongoza waumini wa kanisa hilo(hawapo pichani) katika maombi maalum ya kuliombea Taifa, yaliyofanyika katika ibada Aprili 18, 2020 kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.(wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka).
Baadhi ya waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini, Aprili 18, 2020 wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambapo ameshiriki ibada ambayo waumini hao wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.

Mmoja wa waimbaji wa kwaya ya Kanisa la Waadventista Wasabato Bariadi Mjini akipuliza dawa katika vipaza sauti kuchukua tahadhari dhidi  ya maambukizi ya virusi vya Corona, kwenye ibada ambayo waumini wa Kanisa hilo wameitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa Watanzania wote kuingia katika maombi ya siku tatu ( Aprili 17-19, 2020) kuliombea Taifa ili Mungu aliponye na janga la Corona.

********************************
Mchungaji wa Kanisa la SDA Bariadi Mjini, Marco Mlingwa amesema Kanisa hilo limepokea maelekezo ya Serikali na linaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuliombea Taifa Mungu aliponye na janga la Corona.

Kwa upande wao waumini wa Kanisa la SDA Bariadi Mjini wamemshukuru Mhe. Rais kuruhusu ibada kufanyika kwa kuzingatia maelekezo ya watalaam wa afya na kubainisha kuwa wataendelea kumuomba Mungu aliepushe Taifa na Corona wakiamini kuwa Mungu atasikia wakiomba kwa imani na kwa bidii.

“Tunamshukuru Mhe. Rais kuruhusu ibada kuendelea kufanyika huku tukichukua tahadhari,  sisi Wakristo tunaamini watu tukiomba kwa bidii Mungu anasikia maombi, hivyo tukikutana na kuomba kwa bidii Mungu atasikia na kutuokoa na ugonjwa huu wa COVID 19,” alisema Paul Jidayi muumini SDA na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa.

“Sisi kama Wasabato tuna vipindi vyetu vya afya na kupitia vipindi hivyo tumeshajifunza na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona kanisani na majumbani; pia tunaungana na Rais kuliombea Taifa tukiamini kuwa Mungu atatusikia maana hata zamani, nchi ya Ninawi walipelekewa taarifa kuwa wataangamizwa lakini walipomlilia Mungu aliwasikia na  hawakuangamia,” alisema Mariam Manyangu.

Eliud Rwechungura

WANAWAKE WAJASIRIAMALI WA KARAGWE WAPEWA ELIMU YA BIASHARA NA KUTAMBUA FURSA SHERIA ZA KUFANYA BIASHARA MIPAKANI

    Taasisi ya Mama Alaska Jamii kwa kushirikiana na Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Trade Mark East Africa, Halmashau...